Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

Mwanaume mwenye miaka 60 ajiua kwa kujinyonga wilayani Biharamulo 

Jeshi la Polisi Wilayani Biharamulo wanachunguza tukio la mwanaume mwenye miaka 60 kujiua kwa kujinyonga kwa kujitundika juu ya mti kwa kamba ya katani.


Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Augustine Ollomi amesema marehehmu jina la Marehemu ni William Bizilege, mkazi wa kijiji cha Bisibo wilayani Biharamulo.

Kamanda Ollomi amesema wiki mbili zilizopita marehemu Bizelege alimuua mkewe kisha alikimbilia mafichoni na Jeshi la Polisi lilikuwa likimsaka. Polisi imesema alimuua mkewe sababu ya wivu wa mapenzi.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Askali ajiua kwakujipiga risasi mkoani Mtwara, habari kamili iko hapa

Ni hawa askari wapya waliotoka depo Namba J, watu wanasema saa nyingine alikuwa na matatizo. Inauma sana, inakuaje Askari ajiue mwenyewe?


Lakini kilichonishitua zaidi ni sijaona damu sehemu alipolazwa. Je mtu akifa kwa risasi hatoki damu? Au kuna watu wamemuua. NinaaminJeshi letu la Polisi litatoa habari kamili kuhusiana na hili Swala mapema. Sababu watu washaanza kuongea mengi.


Amejipiga Risasi Mtwara Kusini mwa Tanzania na maiti yake asubuhi hii wanaisafirisha kupelekwa Mwanza ndo kwao. Kwa watu wake wa karibu wanadai alikua hayuko vizuri. Yaani alikuwa kama mtu aliyekuwa anatumia madawa ya kulevya au bangi akaacha. Namba yake ya kazi J PC 734 anaitwa Sengerama.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Vituko vya madreva barabarani, tazama ilivyotokea ajali hii leo

T 602 DGT ni daladala iliyosababisha ajari ambayo inaonekana kwa upande wa kushoto
Na T 436 DFM daladala iliyokuwa kituoni ambayo inaonekana kwa upande wa kulia
Na MC 495 AEQ ndiyo bajaji iliyobaniwa katikati kwenye eneo la kituo cha daladala maeneo ya Kizuiani Mbagala.
Muonekano wa picha za tukio. Mwenye bajaji alidai bajaji yake haikuwa na break 
Eneo la tukio kituoni, napia dreva wa bajaji hii alikuwa ni mremavu alikuwa amewapakia waremavu wenzake wawili jumla walikuwemo ndani ga bajaji hile waremavu watatu.
Abilia wakitazama jinsi tukio lilivyotokea
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Ghala linalomilikiwa na Saba Spare Parts linateketea kwa moto muda huu

Kutoka hapa nilipo naona moshi mkali. Kwa mujibu wa watu waliopo eneo la tukio, wanasema moto unawaka jirani na chuo cha Tumaini kampasi ya Mwenge.


Kinachoungua ni ghala linalomilikiwa na Saba Spare Parts linateketea kwa moto muda huu. Zimamoto wamefika na wanaendelea na uokoaji.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

UNDANI WA HABARI YA KIFO CHA JULIANA ISAWAFO UKO HAPA, BOFYA KWENYE PICHA

Mapema zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii ikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha). 

Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo. 

Hata hivyo Amenithibitishia kwamba Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai. 

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo. 

Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Afariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari Polisi, habari kamili bofya hapa

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Monduli kwaajili ya matibabu. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea usiku maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli. 

“Mara baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa Majengo Moshi ambapo walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung pamoja na fedha taslimu Tsh 50,000/=,” Alisema Kamanda Mkumbo. 


“Wakati wanaendelea na tukio hilo askari Polisi waliokuwa high way patrol walipata taarifa za tukio hilo ambapo walikwenda kwa haraka na mara baada ya majambazi hao kuwaona walianza kufyatua risasi hovyo na polisi kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmoja wao na kuwakamata wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne huku wengine akiwemo na yule mwenye bunduki wakikimbia,” aliongeza. 

Aidha Kamanda Mkumbo alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na bunduki ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na marungu ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo likitokea Moshi kuelekea mkoani Singida. 

Kamanda Mkumbo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa haraka, huku akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila kuvuja jasho kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Wanawake wa 4 na wanaume 9 wafikishwa mahakamani mjini Dodoma kusomewa mashtaka ya mauaji ya watafiti 

Wanawake wanne na wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjini Dodoma na kusomewa mashtaka ya mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi kilichopo Selian mkoani Arusha.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.

Wanadaiwa kuwaua Nicas Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi kwenye Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino.


Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai walitenda kosa hilo la jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na marekebisho yake ya mwaka 2002.

Washtakiwa hao ni Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma Madeha, Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga, Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba, wote wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi.

Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

KUTOKA VIKINDU: Majambazi zaidi ya 10 wakamatwa, wakiwemo askari na Kanali Mstaafu

KUTOKA VIKINDU: Majambazi zaidi ya 10 wakamatwa, wakiwemo askari na Kanali Mstaafu. Imetokea usiku huu Mkuranga. Askari wazingira nyumba ambayo walikuwa wanafanya uchunguzi baada ya mauaji ya polisi Mbande. Radio WAPO.

             ======== UPDATES;========

Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.

Timu ya Mwananchi iliyo eneo la tukio imeshuhudia magari ya polisi (difenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru njia zimefungwa kutokana na mapambano hayo.

Inadaiwa wamekamatwa majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu. Kiongozi wa wahalifu wao anadaiwa kuwa Kanali wa Jeshi mstaafu.

Chanzo: JAMII FORUM

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

KABLA YA AJALI HII KUTOKEA ILIKUWA IVI, BOFYA HAPA KUJUA ZAIDI

Ajali hii imetokea leo maeneo ya Mbagala saba saba kwa Mpili mda wa saa tatu asubuhi
Ilo gari aina ya Rand Lover ndilo limekuja kuivuta iyo daladala kuitoa kwenye eneo la mtaro ilipo angukia.
Hapa unaona raia wakishuhudia ajali hiyo.
Hapa traffic pamoja na raia wakiangalia jinsi ya kuitoa gari hii kwenye eneo hili.
Ilikuwa ni daladala inayofanya safari zake kati ya Tandika na Mbagala rangi tatu, inasemekana imeferi break ndipo ilipo angukia kwenye mtaro wa barabara. 
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

KILICHOMKUTA MCHINA ALIYEMFANYIA UNYAMA MTANZANIA IKI HAPA CHINI

Mchina aliyemfanyia unyama Mtanzania atiwa mbaroni. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba hii leo amewasili mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi kubwa ikiwa ni kufuatia taarifa za mateso na mauaji yaliyofanywa na raia wa china wanaomiliki sehemu ya mgodi wa Nyamhuna uliopo Katoro-Geita dhidi ya wafanyakazi/vibarua ambao ni watanzania.

Takribani wiki moja sasa kumekuwa hali ya sintofahamu dhidi ya picha zinazoenezwa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari zikionesha raia wa tanzania anayefanya kazi kwenye mgodi tajwa akiteswa na kufanyiwa vitendo vya kinyama na mwajili wake ambaye ni raia wa china.

Imemlazimu waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao kupitia wizara ya mambo ya ndani kufika eneo la mgodi kujiridhisha kwa taarifa zilizotapakaa na kubeba simanzi kwa watanzania.

Mwigulu Nchemba amejiridhisha kuwa kulikuwepo na tukio hilo la mtanzania kuteswa na huyo mwajili wake kipigo kilichopelekea kupoteza fahamu na sio kifo.

Hatua za awali mwigulu alizozifanya ni kwenda gereza la Geita mjini alikohifadhiwa kijana huyo kwa madai ameshitakiwa na mwajili wake kwa kosa la wizi lililopelekea yeye kupigwa.

Katika mahojiano ya waziri Mwigulu Nchemba na kijana huyo,Mwigulu alibaini kuwa kijana huyo aliyepo gerezani ndiye mhanga wa tukio lile kwa uthibitisho wa makovu yaliyopo mwili mwake na mavazi aliyovalia wakati anateswa na wakati yupo hapo gerezani.

Katika hali hiyo ilimlazimu Mh.Mwigulu kwenda mgodini akiwa ameambatana na kijana huyo kwaajili ya kutambua waliofanya vitendo hivyo vya kinyama.

Katika oparesheni hiyo, kijana  aliyeteswa na kujeruhiwa aliwabaini watanzania 5 ambao ni walinzi wa eneo hilo na mchina mmoja walioshirikiana kumpiga,kumtesa na kumjeruhi.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

WANANCHI WACHOMA MOTO GARI LA POLISI, HABARI KAMILI IKO HAPA

Habari:Wananchi waokadiriwa kufikia 350 wa kijiji cha Kiangara wilaya ya Liwale mkoani Lindi

wamezikimbia nyumba zao na kutelekeza familia zao kuogopa msako wa polisi wanaowatafuta watuhumiwa waliochoma gari ya polisi wilaya ya Liwale Jumatano iliyopita.

Endelea kuwanasi tukujuze zaidi kupitia hapa hapa kwenye tovuti yako pendwa ya Tazama Line. 
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MORE THAN 10 PEOPLE'S DIED ON MASAKA MBARARA UDANDA, MORE IMAGE GO HERE

The Wreckage on the Masaka-Mbarara highway in which Over 10 people died this evening following an accident involving 4 taxis & trailer.

The accident include this car which have registered to that nomber UAX 781N
Stay with us, we will give you what you want. 

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MTOTO WAMIAKA 7 AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI, ZAIDI BOFYA HAPA

Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza kuwa mnamo tarehe 27.06.2016 majira ya saa 12:00 jioni katika kitongoji cha Moha kijiji cha Ilungu kata ya Nyigogo tarafa ya Itumbili wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mtoto aliyejulikana kwa jina la Julius Leonard miaka [7] mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi ilunga aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake wa kambo aitwaye Leonard Joseph miaka [32] mkulima na mkazi wa kijiji cha Ilunga.

Inadaiwa kuwa marehemu alitumwa na baba yake huyo wa kambo kwenda kuchukua betrii ya simu iliyokuwa imepelekwa kuchajiwa ndipo alichelewa kurudi nyumbani hali iliyopelekea baba yake huyo kuwa na hasira na kuamua kumchapa hadi mtoto huyo akapoteza maisha.

Mwili wa marehemu tayari umefanyiwa uchunguzi wa awali na daktari na kuonekana ukiwa na alama za fimbo huku mguu wa kushoto ukionekana kuvuja damu kwa ndani kutokana na adhabu ya fimbo hizo.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo ametoroka baada ya kuona amefanya mauaji.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana natukio hilo, huku msako wa kumsaka na kumtia nguvuni mtuhumiwa wa mauaji tajwa hapo juu ukiwa unaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa wananchi akiwataka kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi, kwa kutoa taarifa za mtuhumiwa wa mauaji haya mahali alipo ili awezwe kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za aina kama hii.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

WATU 5 WAFARIKI NA 13 KUJERUHIWA MWANZA, CHANZO NI HIKI HAPA

Mnamo tarehe 28.06.2016 majira ya saa 7:00 usiku katika barabara ya Mwanza – Shinyanga eneo la Bushini kata ya Mabuki wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza, gari namba T.449 BCB aina ya Zhongtong mali ya kampuni ya Super Sami lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye William Elias Masa miaka [44] mkazi wa Mabibo Dar es salaam.

Basi hilo likitokea Dar es salaam kwenda Mwanza liligonga jiwe lililokuwa barabarani hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano [5] akiwepo Dereva wa gari hilo na msaidizi wake pamoja na majeruhi kumi na watatu [13].

Taarifa hiyo imewataja waliofariki kuwa ni dereva wa gari hilo aitwaye William Elias miaka [45] mkazi wa Dar es salaam, 2. Vaileth Odede miaka [21] mkazi wa mwanza, 3. Mwanamume mmoja na wanawake wawili wenye umri wa miaka 25-30 ambao majina yao bado hayajatambuliwa mpaka hivi sasa.

Majeruhi kumi na watatu [13] watano kati yao wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu na wengine nane wanaendelea na matibabu katika hospital ya wilaya ya Misungwi ambao ni 1. Sophia Miraji anayekadiriwa kuwa na miaka 20 hadi 25, 2. Kibilo Mwacha anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40, 3. Boniphace Charles anayekadiriwa kuwa na miaka 38 hadi 40, 4. Frank Munyumi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 hadi 30.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi.

Wengine ni 5. Stanley Zacharia anayekadiriwa kuwa na umri kati ya 25 hadi 30, 6. Sia Dauson miaka 28, 7. Hellen Leheke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35, 8. Michael Leonard miaka kati ya 30 hadi 35, 9. Kudra ibrahim mtoto wa miaka miwili na miezi sita, 10.

Zamda issa miaka 24, 11. Marietha Chrispher miaka 26, 12. Elizaberth Simon miaka 40 na 13. Dickson Msamba miaka 22. Majeruhi wote wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Inadaiwa kuwa dereva wa gari hilo alikuwa kwenye mwendo kasi, hali iliyopelekea kugonga jiwe lililokuwa barabarani na kusababisha dereva kushindwa kulimudu basi hilo na kupelekea kuserereka na kuanguka na kusababisha vifo na majeruhi. Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Misungwi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa watumiaji wa vyombo kuwa makini wakati wote pindi wanapokuwa barabarani, lakini pia kuacha kuendesha magari kwa mwendo kasi kwani kunapelekea ajali na vifo vinavyoweza kuepukika.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

BIBI AMUUZA MJUKUU WAKE ALBINO KWA WAUAJI, ZAIDI BOFYA HAPA

Bibi amuuza mjukuu wake albino kwa wauaji huko Busega. Mama mzazi wa mtoto huyo amuokoa na kumnusuru na ukatili ambao ungeliweza kutokea.

Mauaji ya watu wenye ualbino yameota mizizi katika jamii ya Kitanzania na wanaharakati wa haki za binaadamu wameeleza kuwa wimbi hilo limechukua uhai wa Albino sabini na tano nchini Tanzania tangu mwaka wa elfu mbili na viungo vyao kutumika katika masuala ya kishirikina.

Kadhalika, takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa ulemavu mwingine wa kudumu. Source : Jamii Forum. 

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

JAAMANI ULE USEMI WA UKIONA MWENZIO ANAYOLEWA BASI NAWEWE ZAKO TIA MAJI, HUU HAPA

Washtakiwa sita wanaokabiliwa na makosa tofauti yakiwemo ya kubaka, kulawiti na kusambaza picha chafu na za ngono wameendelea kusota rumande kwa kukosa dhamana, baada ya mvutano mkali wa mawakili wa upande wa mashtaka na upande wa washtakiwa kuibuka mahakamani hapo, na hakimu anayesikilisha shauri la dhamana kuahirisha shauri hadi Juni 15 mwaka huu kutoa uamuzi juu ya dhamana.

Miongoni mwa washtakiwa hao, wawili,Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na Zuberi Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya wanaokabiliwa na shtaka la kumbaka na kumlawiti binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami Dakawa,wilayani Mvomero wanalodaiwa kutenda Aprili 27 mwaka huu majira ya usiku katika nyumba ya kulala wageni ya titii iliyopo wami dakawa wilayani mvomero,shauri lao linalosikilizwa faragha limeahirishwa tena mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary Moyo.

Upande wa mashtaka katika shauri hilo linalosikilizwa faragha kwa mujibu wa sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila,Edgar Bantulaki,Calistus Kapinga na Mohamed Mkali na limepangwa kufikishwa tena mahakamani hapo Juni 15 mwaka huu kwaajili ya kuanza usikilizwaji wa awali baada ya upelelezi kukamilika.

Uamuzi wa dhamana itolewe ama isitolewe umeshindwa kufikia muafaka baada ya mvutano wa kisheria wa mawakili wa utetezi na wa Jamhuri, katika shtaka la kusambaza picha chafu na za ngono kwa njia ya mtandao kinyume na sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka 2015, linalosikizwa mbele ya hakimu Ivan Msaki,wa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro,dhidi ya washtakiwa sita,iddi Mabena na Zuberi Thabit,wanaotetewa na wakili Mohamed mkali,na Rajab Salehe,Ramadhani Ally Makunja, Muhsin Ngai na John Peter Thabiti maarufu kama paroko, wakazi wa wami dakawa wilayani Mvomero wanaotetewa na wakili Ignas Punge.

Upande wa mashtaka umeendelea kutetea uamuzi wake wa kuwasilisha kiapo cha kupinga dhamana kwa vile shauri hilo limevuta hisia ya watu, usalama wao utakuwa mashakani wawapo uraiani hasa ikizingatiwa wanadaiwa kudhalilisha utu wa mwanamke na kutoharibu upelelezi kwa vile bado haujakamilika,na kwamba taarifa za kiintelijensia zimebainisha wakiachiwa huru wanaweza wakadhuriwa na jamii.

Hata hivyo upande wa utetezi uliowasilisha hati kupinga kiapo hicho umedai dhamana ni haki ya mshtakiwa,hakuna raia aliyewasilisha kiapo kuhusu hasira kali alizonazo dhidi ya washtakiwa isipokuwa labda ni hisia za mkuu wa upelelezi wa mkoa.

Hakimu Ivan Msaki ameahirisha shauri hilo hadi Juni 15 mwaka huu ambapo uamuzi wa washtakiwa kupewa dhamana au kunyimwa dhamana utajulikana.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

ZAIDI YA MABASI 34 YA MWENDO KASI TAYARI YAMEKWISHA PATA AJALI, ZAIDI BOFYA HAPA

Zaidi ya mabasi 34 katika mradi wa mabasi yanayoenda haraka yamepata ajali kwa kipindi cha siku 20 toka kuanza rasmi mradi huo kutokana na baadhi ya wananchi na madereva wa magari ya kawaida kutumia barabara maalum za mradi wa DART.

Takwimu hizo zimetolewa na meneja uhusiani wa mabasi yao -UDART- Bwana Deus Gugaiwa baada ya kuibuka kwa ajali ya mara kwa mara ambapo amesema ajali hizo zimesababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 94 kwa ajili ya ukarabati hali inayohatarisha uwezekano wa mradi huo kuwaendelevu.

Akielezea hatua zinazochukuliwa dhidi ya wanaoendelea kukiuka sheria, meneja uhusiano wa DART Bwana William Gatambi amesema Dart kwa kushirikiana na jeshi la polisi, wizara ya mambo ya ndani, Tanroad pamoja na jiji la Dar es Salaam wako katika hatua za mwisho za kutayarisha rasimu ya sheria ndogondongo zitakazo toa adhabu kwa wanaokaidi utaratibu wa matumizi sahihi ya miundombinu hiyo Dart.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

GARI AINA YA NOAH YENYE NAMBA T 568 BNZ IMEPATA AJALI MBAYA SANA, BOFYA HAPA

Gari aina ya Toyota Noah yenye namba T568 BNZ imepata ajali mbaya katika barabara ya Mwika - Himo eneo la Makerere

Gari hiyo ilikuwa ikitokea tarakea kuelekea moshi. Idadi kamili ya waliopoteza maisha haijapatikana mara moja. Endelea kuwanasi tukujuze zaidi. 

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

VIFARANGA 500 NA MAYAI YA SAMAKI VYAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA JK NYERERE, ZAIDI BOFYA HAPA

HABARIZAHIVIPUNDE:Serikali yakamata Vifaranga 5000 na mayai ya samaki kutoka nchini Malawi

vyenye thamani ya zaidi ya Millioni 20 katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam, wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MTOTO WA MIAKA 5 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA BRT

Mtoto mmoja ambaye hakuweza kujulikana mara moja jina lake amekufa papo hapo na mama yake kujeruhiwa baada ya kugongwa na basi la mwendo wa haraka

Gari ambalo lilikuwalinatoka Kivukoni kwenda Ubungo wakiwa wamepanda bodaboda katika mataa ya kuongozea magari kwenye makutano ya barabara ya Shekilango na Morogoro jijini Dar es Salaam.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top