Featured

    Featured Posts

Loading...

FAHAMU UGONJWA WA U.T.I, DALILI ZAKE NA JINSI YA KUUEPUKA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

U.T.I (Urinary tract infection) ni ugonjwa wa maabukizi katika mfumo wa mkojo na maambukizi haya yanasababishwa na viumbe kama bakteria,fangasi na virus.

Maranyingi bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo hutolewa na mwili,Wakati mwingine bakteria wanaweza zidi kinga ya mwili na kusababisha maambukizi hayo. U.T.I's inaweza athiri urethra,kibofu cha mkojo na figo.

MFUMO WA MKOJO
Mfumo wa mkojo ni mfumo wa mwili unaotumika kuondoa uchafu na maJi ya ziada, Mfumo huu unaundwa na ureta, kibofu cha mokojo,figo na urethra sitachambaua kwa undani hizi sehemu.

Mara nyingi U.T.I zinasababishwa na bakteria aitwaye Escherichia coli (E. coli) na U.T.I nyingine zinaweza sababishwa na Chlamydia na Mycoplasma na U.T.I hizi zina athiri hadi mfumo wa uzazi na wanandoa wanapaswa kupata tiba pamoja,Maambukizi ya U.T.I ni makubwa sana dunian Zaidi ya watu milioni 8.1 wanaathiriwa na ugonjwa huu.

WANAWAKE NDO WAHANGA WAKUBWA
Wanawake ni wahanga wakubwa sana wa ugonjwa huu kulingana na maumbile yao ya nje.

1.Urethra(mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu) kwa wanawake ni mfupi sana hivyo kuruhusu bakteria kufika kwa haraka kwenye kibofu

2.Pia mrija huo unafungukia sehemu ambazo zinaweza kuwa ni vyanzo vya bakteria ambayo ni sehemu ya uke na pili ni puru ila Kwa wanaume ni vigumu sana ila wakipata tatizo linaweza kuwa zito kutibu tofauti na kwa wanawake.

Watu walioko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu wa U.T.I ni wale Watu wenye vidonda kwenye uti wa mgongo, Mtu yeyote mwenye tatizo katika mfumo wa mkojo, pia na Tendo la ndoa linaweza likahamisha bakteria kutoka kwenye uke kwenda kwenye urethra na Baadhi ya njia za uzazi kama kutumia diaphragm,spermicides,kondomu nk.

KURUDIARUDIA KWA UTI(UTI SUGU)
Mara nyingi wanawake wakipata U.T.I inaweza ikawa inajirudia mara kwa mara kulingana na sababu kama zifuatazo;

1.Uwezo wa bakteria kujishika kwenye njia ya mkojo hivyo kutotibika na kurudia tena, na pia

2.Sababu nyingine ni wanawake kuwa non sector yani kuwa na damu grupu A,B na AB ambao hawawezi kuzalisha kinga nzuri kwa ajili ya hao bakteria.

DALILI ZA U.T.I
1.Kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati wa kukojoa.

2.Kuhisi kuunguzwa na mkojo kwenye kibofu au mrija wa mkojo.

3.Maumivu ya misuli na tumbo
4.Mkojo kuwa na harufu mbaya na pia kubadilika rangi kuwa nyeusi au rangi ya mawingu nk.

5.Kwa mtu aliyeathiriwa figo anaweza kuwa na maumivu mgongoni au kwenye mbavu pia kichefuchefu na kutapika.

6.Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo kidogo uku unapata maumivu kwenye njia ya kupitisha mkojo.

JINSI YA KUZUIA U.T.I SUGU
1.Kunywa maji mengi kunsaidia kusafisha bakteria kwenye mfumo wa njia ya upitishaji wa mkojo.

2.Mtu anatakiwa akojoe mara kwa mara kila anapojiskia kukojoa, usibane mkojo maana Mkojo ukikaa sana kwenye kibofu unaweza zalisha bakteria.

3. Na baada ya kukojoa wanawake wanatakiwa kujisafisha kuanzia mbele kurudi nyuma ili kulinda urethra, (Msisitizo, wanawake wengi wanakosea kwenye wakati wa kujisafisha baada ya kumaliza kukojoa)

4.Vaa nguo za ndani za pamba na ambazo hazibani sana kuruhusu hewa kupita vizuri, epuka nguo aina ya jinsi zinazobana sana ambazo zinaweza kukusanya jasho kisha kuleta tatizo.

5.Kwa akina mama/dada watumie ped za neplily ped pekee zenye uwezo wa kuzuia na kutibu U.T.I na pia zinaruhusu hewa kupita vizuri na kuimalisha usalama wao.

MATIBABU YA U.T.I SUGU
Tumia package yetu ya siku 90 ANTI-UTI PACKAGE package yenye dawa ya kuondoa tatizo la U.T.I sugu pamoja na pedi zake ambayo itakusaidia kuondokana na tatizo hilo package ambayo imesaidia wengi na inazidi kutoa ushuhuda kwa jamii (pedi ni option kutokana na jinsia)

Kwa ushauri na matibabu wasiliana nami
+255 656459057
Whatsapp +255 656459057
Koroti Mwashungu
Health Consultant

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Chapisha Maoni

CodeNirvana
Inaendeshwa na Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top