Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.
Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara
Chumvi
Mchele
Sukali

Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari
Vichongeo

Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka

Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria
Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati

Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kazole achunguzwe na ikiwezekana aachie ngazi.

Kazole ni kijiji kinachopatikana kwenye kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Kijiji hiki kinaundwa na vitongoji kama Ngunguti, Cheta, Kilongoni nk.
Picha izi zote ndizo zinazo onyesha uharisia wa barabara kuanzia Vikindu kupitia Kazole kwenda mpaka Cheta na mwisho wake ni Magodani pamoja na maeneo mengineyo kama Kimbiji nk.

Mwenyekiti wa Kazole achunguzwe na ikiwezekana aachie ngazi, pia Viongozi wote wa vitongoji vinavyounda kijiji hiki wachunguzwe mali zao au waache kazi.

Yote haya nikutokana na utendaji wao wa kazi katika maeneo yao wanayo yaongoza hapa kazole, cheta, kilongoni, pamoja na maeneo mengine yanayounda kijiji cha Kazole na majirani zetu wakazi wa Magodani.

 Toka Kazole iwe kijiji mwaka 2013 mpaka leo mwaka 2017 hakuna ofisi rasmi ya kijiji iliyojengwa kwa pesa ya kutoka kwenye mfuko/akaunti ya kijiji zaidi ya kukodi frem ili kuweka ofisi mahari hapo.

Watu wananunua viwanja na wanalipa 10% (asilimia 10) ya manunuzi yao kwenye ofisi ya kijiji ila pesa izo hazionekani zinapokwenda.

Mikutano ya vitongoji au kijiji ufanyika lakini kwenye kipengere cha mapato na matumizi kila kiongozi ushikwa na kigugumizi na kushindwa kutoa majibu sahihi kwa wananchi pale wanapo hoji.

Pesa pekee ya makusanyo ya mauzo ya viwanja kwa mwaka mmoja kwenye kijiji hiki cha Kazole zinatosha kabisa kujenga ofisi ya kijiji, pamoja na kwamba kijiji ndo kinakua ila kila mwaka tunaweza kujenga ofisi ndogo moja kwa kila kitongoji.

Mauzo ya viwanja kwa mtu mmoja mmoja na michango mbali mbali kutoka kwa wananchi pamoja na wadau zitumike ipasavyo ili kuleta maendeleo ya wananchi.

Pesa zote izi za mauzo ya viwanja, michango ya wananchi pamoja na michango ya wadau zilianza kuliwa na viongozi hao tangu na kabla Kazole haijawa Kitongoji mpaka leo.

Hadi sasa kijiji pamoja na vitongoji vyake hakuna Barabara nzuri na zenye uakika wa kupitika kwa masaa 24 kwa mwaka mzima, Umeme, Makanisa, Misikiti ipo kwa baadhi tu ya maeneo, Hospital au Zahanati, Shule ya msingi bora pamoja na Sekondari, maeneo rasmi ya Masoko, Maziko, Michezo nk.

Kazole shule ya msingi mpaka sasa haijafikisha hata madarasa 7 ya kuwafundishia watoto wa elimu ya msingi, na shule ya sekondari ni moja tu ambayo ni Honda sekondari school.

Ambapo ni umbali mkubwa sana kwa watoto wanaotoka kazole, cheta, magodani na kilongoni kwenda kupata elimu kwenye shule iyo,  pia shule hii ya Honda secondary sio shule ya kijiji cha kazole pamoja na vitongoji vyake bali ni shule ya majirani zetu wa Vianzi.

Kwaiyo basi, kuna haja ya serikali ya kijiji kutenga rasmi maeneo yaliyotajwa pamoja na kuhakikisha yanatumika hipasavyo ili kuchochea ukuaji wa maendeleo ya kijiji.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MKOMBOZI WA NYATI CEMENT INDUSTRY NI BARABARA YA VIKINDU GETINI KUPITIA KAZOLE, CHETA, MAGODANI, MWASONGA HADI KIMBIJI.

Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.

Kimbiji kuna muwekezaji wa kiwanda cha Nyati cement ambapo katika utoaji wa huduma yake kwa watanzania hulazimika kutumia barabara ya Kibada uku Kigamboni ili kusafirisha cement kutokea Kimbiji hadi mjini.

Lakini kuna barabara ambayo ni fupi sana kuliko ile anayoitumia muwekezaji uyo wa kiwanda cha Nyati Cement kwa sasa.

Barabara iyo fupi inayozungumziwa ni ile inayoanzia Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji na kuunganisha maeneo mbali mbali ya katikati ambayo ayajatajwa.

Kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutampunguzia muwekezaji huyu adha ya usafirishaji wa Cement yake na kumuongezea nguvu ya kuzalisha cement nyingi zaidi.

Pia kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutatoa fursa kwa wakazi wa maeneo tajwa kukua kibiashara, kiuchumi ata kisiasa nk.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.


Kwa sasa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji ipo kama unavyo iona kwenye picha hapo juu na chini.

Pia wakazi wa maeneo tajwa wanapata shida sana katika kusafiri, ambapo kutoka Vikindu getini hadi Kazole magenge 20 ni umbali wa dakika 15 hadi 20 ila kila abiria hutozwa Tsh. 500 na mwanafunzi tsh. 200 hadi tsh. 250.

Huku Noah zinazoanzia Vikindu getini kwenda hadi Magodani zikipitia Kazole magenge 20 pamoja na Cheta kila abiria anatozwa Tsh. 1,000 ukiwa ni umbali wa kama dakika 30 hadi 35 tu.

Izo bei za nauri hutozwa kipindi cha kiangazi ila ikifika masika nauri upanda hadi mara 4, wakazi wa Kazole ulipa tsh. 2,000 na wakazi wa Cheta na Magodani ulipa tsh. 4,000 na Boda boda uwa ni kati ya tsh. 5,000 mpaka tsh. 10,000

Lakini mbali ya nauri kuwajuu namna hiyo japo sio viwango elekezi kutoka SUMATRA, bado kuna changamoto ya uchache wa magari yanayotoa huduma, kwaiyo tunamuomba Mhe. Rais Magufuri na serikari yake kupitia wizara ya ujenzi walitazame swala hili kwa jicho la tatu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu kufanyiwa ukarabati

Mkuu wa wilaya azungumzia barabara ya Magodani na Kilongoni hadi Vikindu inayopitia Cheta, Kazole kisha kuunganisha kwenye barabara kuu ya rami inayoenda mikoa ya kusini.
Barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu kufanyiwa ukarabati
Barabara ya Magodani, Cheta, Kazole, Kilongoni hadi Vikindu kufanyiwa ukarabati

Habari kamili isome kupitia
[HAPA] 


Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

WAKAZI WA CHETA WANATAKA BARABARA, SHULE, UMEME, SOKO, HOSPITAL, MAJI, MSIKITI NA KANISA

Maendeleo huletwa na watu, watu wenyewe ndio sisi tukishirikiana na viongozi wetu ndipo tunaweza kupiga hatua chanya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa


Ila wazo ili naona linapingana na uhalisia wa maisha ya wananchi na wakazi wa eneo la Cheta pamoja na viunga vyake.

Ikiwa imepita miezi michache ndani ya mwaka huu wa 2017 tayari zimeonekana alama za vijiti zinazo ashiria njia za uwekaji wa nguzo za umeme.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa

Alama izo zimetokea eneo la Vikindu zimepita eneo la Kazole mjini, Kazole shule ya msingi iliyopo mpakani na eneo la Hamidu na nguzo ya mwisho imeishia Kazole Magenge 20 eneo la njia panda ya kwenda kwa Bakhresa ambapo ndipo mpakani mwa Kazole na Cheta.

Sasa kuanzia hapo mpakani mwa Cheta na Kazole kwenda hadi mpakani mwa Cheta na Magodani hakuna alama yoyote inayo onyesha kuwa nguzo za umeme zitapita ili kwenda mpaka Magodani.

Cheta ipo ndani ya Kazole uku ikipakana na Magodani ila viongozi wa kazole kwa ujumla wamekuwa wakipasahau sana Cheta.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa


Baada ya uongozi wa Magodani kuchonga barabara yao kuanzia mpakani mwa Cheta kuelekea kwao ndipo Kazole wao walisimika alama za kuonyesha njia za nguzo za umeme zitakapo pita na wao wakaishia mpakani mwa Kazole na Cheta

Je Cheta inayoachwa katikati inaongozwa na akina nani?? Na je kama ina viongozi wake ivi wao wanatambulika upande wa Magodani au upande wa Kazole?? Wananchi wanataka kufahamu.

Kumbuka wakazi wote wa maeneo ya Mwasonga, Magodani, Cheta, Kazole na Vikindu wanategemea Barabara inayoanzia Vikindu hadi uko Mwasonga pamoja na maeneo mengine ambayo sikuyataja sasa je kama maendeleo na miundo mbinu vinawekwa mwanzoni mwa eneo na mwishoni bila kupaunganisha katikati je kunatengeneza kitugani jamani??
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa



Wananchi wa Cheta wanataka maendelea ya kweli kwa vitendo nasio maendeleo ya kuongea mdomoni na kuwadanganya kwenye mikutano ya vijiji inayofanyika.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara safi, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.

Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule ya msingi na ya Sekondari, Hospital, Soko, Umeme, Visima vya Maji masafi, Viwanja vya Michezo, Sehemu za ibada (Miskiti/Makanisa), Maziko nk.
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa
Wakazi wa Cheta wanataka Barabara, Shule, Umeme, Soko, Hospital, Maji, Msikiti na Kanisa



Kwa habari zaidi juu ya wakazi wa Cheta, Kazole na Magodani tazama apo chini.

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WAKAZI WA KIJIJI CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE ZIKO HAPA
             [Bofya hapa kusoma]


ILE BARABARA INAYOANZIA VIKINDU GETINI KWENDA HADI MAGODANI NDIO HII
              [Bofya hapa kusoma]


KUTOKA PWANI: HIKI NDICHO KIJIJI CHA KAZOLE PAMOJA NA VITONGOJI VYAKE
              [Bofya hapa kusoma]


CHANZO CHA KUZOROTA KWA MAENDELEO KWENYE KIJIJI CHA KAZOLE NA VITONGOJI VYAKE IKI HAPA
           [Bofya hapa kusoma]


ENEO LA HEKARI 2 LINAUZWA, LIPO KWENYE KIJIJI CHA CHETA
                [Bofya hapa kusoma]

ENEO LA HEKARI 17 LINAUZWA / 17 HECTARES FOR SALE, GO HERE NOW
            [Bofya hapa kusoma]

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Kutoa mimba akukufanyi kuendelea kuwa binti bali unabaki kuwa mama wa marehemu

Kutoa mimba akukufanyi kuendelea kuwa binti bali unabaki kuwa mama wa marehemu (i-save iyo).
Hii picha ni kwa hisani ya Rose Muhando kwenye wimbo wa Yesu ni wetu
kwa habari mbali mbali usisite kutembelea MUTALEMWA BLOG na MIKOA YETU
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari

Heshima Kwenu wakuu, Leo nimeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.

Karibuni.

=======

UPDATES;


=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.
Nape anaongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli akiwa juu ya gari

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu.


Mimi ndo nimekuwa mzalendo kwa CCM, ambayo niliikuta ikiingia kwenye shimo inakwenda, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, na nilichokisiamamia juzi ni kusema kweli, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, kamaninachokiamini kitaleta matatizo mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepanda mbegu ya kupigania haki hakika itaota, Tanzania ni yetu nchini yetu. Vijana hamna la kuogopa simamieni mnachokiamini Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.

Sisi pia tutaondoka suala la kujiuliza tutaawaachia watoto wetu nchi ya aina gani, hilo ndio kubwa,uamuzi ni wa kwetu wenyewe

Lengo la kuja hapa ni kumshukuru Rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari. 

Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli ndiye rais tuliyenaye na kudumisha umoja na mshikamano.

Tumefanya kazi pamoja na nimefurahi sana kufanya kazi na nyie 
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia. Niliomba kazi ya Ubunge na sio uwaziri, sasa narudi kuwatumikia wananchi wangu wa Mtama 

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni. Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Rais Magufuli afuta Agizo la Kufunga Ndoa kwa Sharti la kuwa na Vyeti vya Kuzaliwa.

Mbali ya maelezo mengi aliyoyatoa Mhe.Rais pia amesema kuwa vyeti vya kuzaliwa vilianza kutolewa baada ya nchi yetu kupata uhuru.

Pia ameeleza kuwa mpaka sasa watanzania wenye vyeti vya kuzaliwa hawafiki asilimia 20%

Kwaiyo hatuwezi kuwa na sheria ya kuwabagua watanzania

Pia akaongeza kusema kwamba kuna aja ya wanasheria wetu kuangalia upya sheria ya vizazi na vifo pamoja na sheria ya ndoa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionesha majina mengine 97 ya wauza  Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya,

Bw. Rogers William Sianga   ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu  hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,


 ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC


Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Waliotajwa live na mkuu wa mkoa wa Dsm mh.Paul Makonda hawa hapa

Aliyozungumza Makonda mchana huu na waandishi wa habari!.
Anasema anaingia awamu ya pili ya mapambano ambayo siyo nyepesi,anasema itakuwa na mawimbi mengi!.

1.Yanaingizwa kutoka Pakistan kwa meli,ikishapakia mzigo wanachukua madawa kwenye mifukonya sukari inawekwa kwenye mapipa!

Meli zikikaribia kufika mapipa hutupwa huko Zanzibar,Tanga na Bagamoyo yakiwa na GPRS,baadae hurudi walipoyatupa na kuyachukua na huyasafirisha mpaka Mtwara na baadae Afrika kusini!.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

BARABARA INAYOANZIA VIKINDU GETINI HADI MAGODANI NDIO HII

Maendeleo hayana chana wala dini, karibu ndugu msomaji wetu.
Barabara hii ina wastani wa 10km kwa makadirio, barabara hii inaanzia eneo la Vikindu Getini wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, inapitia kijiji cha Kazole kisha kitongoji cha Cheta na kuendelea hadi kijiji cha Magodani na kuunganisha maeneo mengineyo huko mbele.
Apa ndipo vikindu getini ambapo barabara hii uanzia.

Nauri yake kwenda/kurudi ni Tsh 1,000 kwa mtu mzima na Tsh 500 kwa mwanafunzi.

Kwa sasa wakazi wa Kazole, Cheta pamoja na Magodani usafiri wao mkubwa ni magari aina ya Noah ambazo upaki Vikindu, japo kuna daradara tatu zinazotoa huduma kuanzia Mbagala rangi tatu hadi Kazole Magenge 20 nazo hutoza nauri ile ile, ila ikifika kipindi cha masika tu basi magari hayo yote hayatoi huduma tena.

Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba miundombinu yake ni mibovu kupitiliza, barabara hii kuchongwa yote kuanzia Vikindu hadi Magodani na kuwekwa kifusi pamoja na kurekebisha mitaro pamoja na madaraja yake yote imekuwa kitendawili.

Mwaka 2016 katikati kulitengenezwa madaraja mawili madogo ambayo yapo hadi sasa, daraja la kwanza lipo Mkokozi wa kwanza na lapili lipo Mkokozi wa pili, maeneo haya ni mikondo ya Maji, majibu yake tunayasubili kwenye kipindi cha masika kinachokuja maana ni wazi kabisa kwamba madaraja hayo hayawezi kumudu mshindo wa maji katika maeneo hayo.

Barabara hii ni yamuhimu sana maana ndio barabara pekee inayotumiwa na watu wengi kutoka maeneo mbali mbali.

Changamoto ni nyingi wanazokumbana nazo wakazi wa maeneo tajwa, mpaka sasa hawajafikiwa na umeme, maeneo yao hayaja pimwa, hawana maji safi, hospital, shule za secondary, sehemu za ibada, masoko, maeneo ya michezo, maziko, nk.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

EWURA YAPIGWA STOP NA WAZIRI MUHONGO KUTOPANDISHA BEI YA UMEME, BOFYA HAPA

 EWURA YAPIGWA STOP NA WAZIRI MUHONGO: Tumepokea taarifa za barua ya leo, 31 Dec 2016 kutoka kwa Prof Muhongo kwenda kwa DG EWURA ikisimamisha utumiaji wa bei mpya zilizotangazwa jana na EWURA.
Prof Muhongo ametumia madaraka aliyopewa na yako ndani ya Electricity Act, 2008. Serikali haijapokea na kutathmini bei zilizopendekezwa na EWURA. Uchumi wa viwanda unahitaji umeme wa bei nafuu. 
VIVA TANZANIA


Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

KATUNI YA SIKU: KURE MWISHO NANI BADO HAJAISOMA NAMBA??


KATUNI YA SIKU: KURE MWISHO NANI BADO HAJAISOMA NAMBA??
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Kama wewe ni mvutaji wa sigara, basi usisite kusoma habari hii

Tazama picha izi mbili kisha angalia utofauti iliopo kati ya picha namba moja na picha namba mbili.
Inasadikika kwamba watu wote wanaotumia sigara, maarufu kama wavutaji sigara wako hatarini kujipoteza wao wenyewe kutomana kujiunguza mfumo wao wa mwili.
Picha unayoiona hapo kwa upande wako wa kushoto inaonyesha hali halisi ya muonekano wa mtu kwa ndani jinsi mfumo wake ulivyo salama ukiachilia mbali magonjwa kama Ukimwi na kadhalima, picha unayoiona hapo kulia kwako ndivyo mvutaji wa sigara anavyo onekana kwa ndani.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top