Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MINI SHOP CHETA

Mini ShopCheta au Duka Dogo

Ni duka dogo kweli kama jina lake linavyojieleza hapo juu. Duka hili linatoa huduma ya mahitaji ya kawaida ya kila siku kwa wakazi wa Kitongoji cha Cheta pamoja na maeneo ya jirani au kwa lugha nyingine tunaweza kusema Mini Shop inatoa huduma ya jamii kwa watu wote. Mini Shop ilianzishwa tangu mnamo tarehe 18/01/2018.

Tulianza tunauza bidhaa chache sana, bidhaa izo ilikuwa ni pamoja na Dawa ya Mbu zile za vidonge za kuchoma, Viberiti, Karanga, Ubuyu pamoja na Tauro za wanawake (Ped). Na kipindi icho tulikuwa tunauza bidhaa izo kutokea nyumbani kabla ya kujenga Frem hii rasmi ya kufanyia biashara kama inavyo onekana hapo kwenye picha.
Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mini Shop a.k.a Duka Dogo tunauza bidhaa mbali mbali ila kwa ucheche tu, zifuatazo ni baadhi ya bidhaa tunazouza. 

Maji
Pipi
Unga
Tambi
Ngano
Amira
Juice
Mikate
Sigara
Chumvi
Mchele
Sukali

Karamu
Battery
Viwembe
Vitunguu
Viberiti
Biscuits
Madaftari
Vichongeo

Majani ya Chai
Dawa ya Mswaki
Jumbo Ball Gum
Sabuni za kuogea
Mafuta ya kupaka

Viungo vya Pirau
Mafuta ya kupikia
Sabuni za kufuria
Maharage ya Njano
Maharage ya Kombati

Tauro za wanawake (Ped)
Pon Pon au Bambino za watoto wachanga
Pia Mini Shop ni wakala wa Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Karibu sana dukani kwetu, karibu sana Mini Shop_Cheta tukuhudumie leo.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

NYUMBA PAMOJA NA FREMU ZA BIASHARA ZINAUZWA

Nyumba hii ina idadi ya vyumba vitano (5) ambavyo unaweza kuvitumia kwenye matumizi yako binafsi kulingana na jinsi unavyotaka kutumia sehemu ya vyumba ivyo.
Cheta kwa Kijonjo

ipo karibu na barabara kuu ya serikari, kwaiyo inafaa sana kwa biashara pamoja na makazi ya kawaida tu ya kila siku kama kulala pamoja na huduma zingine.
Cheta kwa Kijonjo.

tayari imeisha fanyiwa wireling (mfumo wa umeme upotayari) kinachosubiliwa ni umeme kuwashwa tu basi alafu matumizi yaanze.
Cheta kwa Kijonjo frem

Kuhusu huduma ya maji ondoa shaka maana kisima kimechimbwa nyuma ya fremu/nyumba hii, pia eneo iloilo kuna huduma ya tofari, mchanga, cement, kokoto, nk.
Cheta kwa Kijonjo house

Nyumba hii au frem hii, ipo kijiji cha Kazole kitongoji cha Cheta kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. 

Bei ni tsh 24,000,000/- (millions ishirini na nne) pia mazungumzo yapo.

Mawasiliano:
0659 91 9292
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MFANYA BIASHARA WA KWELI LAZIMA AJIZUE NJIA IZI

Mpenzi msomaji wa makala hii, napenda nikwambie kitu kwamba siku izi watu wengi wanapenda kuanzisha biashara zao binafsi uku lengo lao kuu nikuachana na kuajiliwa kisha wajiajiri wenyewe na kujipatia kipato kupitia biashara zao walizo zianzisha.

Biashara za kufanya ziponyingi sana hapa duniani,ambazo ukizisimamia vizuri zinakutimizia marengo yako.

Mini Shop_Cheta kwa wakala_Mutalemwa

Mbali ya kwamba biashara nyingi zenye faida ya haraka ni zile biashara ambazo zina madhara makubwa kwa afya wa wanadamu mfano waweza kuwa Sigara, Pombe, madawa ya kulevya nk.

Ila zipo biashara ambazo nazo zinakuwa na faida japo kuwa inapatikana taratibu na uchukua mda mrefu kidogo kuonekana tofauti na biasha nilizo tangulia kuzitaja hapo juu.

Biashara izo ni pamoja na Unga wa Sembe, Sukari, mafuta ya kula, Pipi, jojo, soda, maji, madaftari, karamu, nk. Sasa basi, ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yako yoyote ile utakayokuwa umeichagua kuianzisha unatakiwa kuwa na mipango mazubuti juu ya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.

Mini Shop+Cheta+kwa wakala+Mutalemwa

Mipango iyo nipamoja na kujua namna ya kutenganisha faida na pesa ya mtaji, kuweza kujua namna ya kuendesha mfumo mzima wa mauzo pamoja na manunuzi, kulipa mishahara nk.

Angalizo, huwezi kufanya biashara bila kumbukumbu, biashara yoyote ile inahitaji utunzaji wa kumbukumbu, usipoweza kipengele hiki basi jua kabisa wewe huwezi kufanya biashara yenye tija, bali unaweza kufanya biashara ya mazoea tu basi. Kujaribu sio kushindwa ebu anza leo uone miujiza ya biashara.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kazole achunguzwe na ikiwezekana aachie ngazi.

Kazole ni kijiji kinachopatikana kwenye kata ya Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani. Kijiji hiki kinaundwa na vitongoji kama Ngunguti, Cheta, Kilongoni nk.
Picha izi zote ndizo zinazo onyesha uharisia wa barabara kuanzia Vikindu kupitia Kazole kwenda mpaka Cheta na mwisho wake ni Magodani pamoja na maeneo mengineyo kama Kimbiji nk.

Mwenyekiti wa Kazole achunguzwe na ikiwezekana aachie ngazi, pia Viongozi wote wa vitongoji vinavyounda kijiji hiki wachunguzwe mali zao au waache kazi.

Yote haya nikutokana na utendaji wao wa kazi katika maeneo yao wanayo yaongoza hapa kazole, cheta, kilongoni, pamoja na maeneo mengine yanayounda kijiji cha Kazole na majirani zetu wakazi wa Magodani.

 Toka Kazole iwe kijiji mwaka 2013 mpaka leo mwaka 2017 hakuna ofisi rasmi ya kijiji iliyojengwa kwa pesa ya kutoka kwenye mfuko/akaunti ya kijiji zaidi ya kukodi frem ili kuweka ofisi mahari hapo.

Watu wananunua viwanja na wanalipa 10% (asilimia 10) ya manunuzi yao kwenye ofisi ya kijiji ila pesa izo hazionekani zinapokwenda.

Mikutano ya vitongoji au kijiji ufanyika lakini kwenye kipengere cha mapato na matumizi kila kiongozi ushikwa na kigugumizi na kushindwa kutoa majibu sahihi kwa wananchi pale wanapo hoji.

Pesa pekee ya makusanyo ya mauzo ya viwanja kwa mwaka mmoja kwenye kijiji hiki cha Kazole zinatosha kabisa kujenga ofisi ya kijiji, pamoja na kwamba kijiji ndo kinakua ila kila mwaka tunaweza kujenga ofisi ndogo moja kwa kila kitongoji.

Mauzo ya viwanja kwa mtu mmoja mmoja na michango mbali mbali kutoka kwa wananchi pamoja na wadau zitumike ipasavyo ili kuleta maendeleo ya wananchi.

Pesa zote izi za mauzo ya viwanja, michango ya wananchi pamoja na michango ya wadau zilianza kuliwa na viongozi hao tangu na kabla Kazole haijawa Kitongoji mpaka leo.

Hadi sasa kijiji pamoja na vitongoji vyake hakuna Barabara nzuri na zenye uakika wa kupitika kwa masaa 24 kwa mwaka mzima, Umeme, Makanisa, Misikiti ipo kwa baadhi tu ya maeneo, Hospital au Zahanati, Shule ya msingi bora pamoja na Sekondari, maeneo rasmi ya Masoko, Maziko, Michezo nk.

Kazole shule ya msingi mpaka sasa haijafikisha hata madarasa 7 ya kuwafundishia watoto wa elimu ya msingi, na shule ya sekondari ni moja tu ambayo ni Honda sekondari school.

Ambapo ni umbali mkubwa sana kwa watoto wanaotoka kazole, cheta, magodani na kilongoni kwenda kupata elimu kwenye shule iyo,  pia shule hii ya Honda secondary sio shule ya kijiji cha kazole pamoja na vitongoji vyake bali ni shule ya majirani zetu wa Vianzi.

Kwaiyo basi, kuna haja ya serikali ya kijiji kutenga rasmi maeneo yaliyotajwa pamoja na kuhakikisha yanatumika hipasavyo ili kuchochea ukuaji wa maendeleo ya kijiji.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

MKOMBOZI WA NYATI CEMENT INDUSTRY NI BARABARA YA VIKINDU GETINI KUPITIA KAZOLE, CHETA, MAGODANI, MWASONGA HADI KIMBIJI.

Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.

Kimbiji kuna muwekezaji wa kiwanda cha Nyati cement ambapo katika utoaji wa huduma yake kwa watanzania hulazimika kutumia barabara ya Kibada uku Kigamboni ili kusafirisha cement kutokea Kimbiji hadi mjini.

Lakini kuna barabara ambayo ni fupi sana kuliko ile anayoitumia muwekezaji uyo wa kiwanda cha Nyati Cement kwa sasa.

Barabara iyo fupi inayozungumziwa ni ile inayoanzia Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji na kuunganisha maeneo mbali mbali ya katikati ambayo ayajatajwa.

Kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu Getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutampunguzia muwekezaji huyu adha ya usafirishaji wa Cement yake na kumuongezea nguvu ya kuzalisha cement nyingi zaidi.

Pia kuimarika kwa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji kutatoa fursa kwa wakazi wa maeneo tajwa kukua kibiashara, kiuchumi ata kisiasa nk.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.
Cheta: Mkombozi wa Nyati Cement Industry ni barabara ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji.


Kwa sasa barabara hii ya Vikindu getini kupitia Kazole, Cheta, Magodani, Mwasonga hadi Kimbiji ipo kama unavyo iona kwenye picha hapo juu na chini.

Pia wakazi wa maeneo tajwa wanapata shida sana katika kusafiri, ambapo kutoka Vikindu getini hadi Kazole magenge 20 ni umbali wa dakika 15 hadi 20 ila kila abiria hutozwa Tsh. 500 na mwanafunzi tsh. 200 hadi tsh. 250.

Huku Noah zinazoanzia Vikindu getini kwenda hadi Magodani zikipitia Kazole magenge 20 pamoja na Cheta kila abiria anatozwa Tsh. 1,000 ukiwa ni umbali wa kama dakika 30 hadi 35 tu.

Izo bei za nauri hutozwa kipindi cha kiangazi ila ikifika masika nauri upanda hadi mara 4, wakazi wa Kazole ulipa tsh. 2,000 na wakazi wa Cheta na Magodani ulipa tsh. 4,000 na Boda boda uwa ni kati ya tsh. 5,000 mpaka tsh. 10,000

Lakini mbali ya nauri kuwajuu namna hiyo japo sio viwango elekezi kutoka SUMATRA, bado kuna changamoto ya uchache wa magari yanayotoa huduma, kwaiyo tunamuomba Mhe. Rais Magufuri na serikari yake kupitia wizara ya ujenzi walitazame swala hili kwa jicho la tatu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top