Picha izi zote ndizo zinazo onyesha uharisia wa barabara kuanzia Vikindu kupitia Kazole kwenda mpaka Cheta na mwisho wake ni Magodani pamoja na maeneo mengineyo kama Kimbiji nk.
Mwenyekiti wa Kazole achunguzwe na ikiwezekana aachie ngazi, pia Viongozi wote wa vitongoji vinavyounda kijiji hiki wachunguzwe mali zao au waache kazi.
Yote haya nikutokana na utendaji wao wa kazi katika maeneo yao wanayo yaongoza hapa kazole, cheta, kilongoni, pamoja na maeneo mengine yanayounda kijiji cha Kazole na majirani zetu wakazi wa Magodani.
Toka Kazole iwe kijiji mwaka 2013 mpaka leo mwaka 2017 hakuna ofisi rasmi ya kijiji iliyojengwa kwa pesa ya kutoka kwenye mfuko/akaunti ya kijiji zaidi ya kukodi frem ili kuweka ofisi mahari hapo.
Watu wananunua viwanja na wanalipa 10% (asilimia 10) ya manunuzi yao kwenye ofisi ya kijiji ila pesa izo hazionekani zinapokwenda.
Mikutano ya vitongoji au kijiji ufanyika lakini kwenye kipengere cha mapato na matumizi kila kiongozi ushikwa na kigugumizi na kushindwa kutoa majibu sahihi kwa wananchi pale wanapo hoji.
Pesa pekee ya makusanyo ya mauzo ya viwanja kwa mwaka mmoja kwenye kijiji hiki cha Kazole zinatosha kabisa kujenga ofisi ya kijiji, pamoja na kwamba kijiji ndo kinakua ila kila mwaka tunaweza kujenga ofisi ndogo moja kwa kila kitongoji.
Mauzo ya viwanja kwa mtu mmoja mmoja na michango mbali mbali kutoka kwa wananchi pamoja na wadau zitumike ipasavyo ili kuleta maendeleo ya wananchi.
Pesa zote izi za mauzo ya viwanja, michango ya wananchi pamoja na michango ya wadau zilianza kuliwa na viongozi hao tangu na kabla Kazole haijawa Kitongoji mpaka leo.
Hadi sasa kijiji pamoja na vitongoji vyake hakuna Barabara nzuri na zenye uakika wa kupitika kwa masaa 24 kwa mwaka mzima, Umeme, Makanisa, Misikiti ipo kwa baadhi tu ya maeneo, Hospital au Zahanati, Shule ya msingi bora pamoja na Sekondari, maeneo rasmi ya Masoko, Maziko, Michezo nk.
Kazole shule ya msingi mpaka sasa haijafikisha hata madarasa 7 ya kuwafundishia watoto wa elimu ya msingi, na shule ya sekondari ni moja tu ambayo ni Honda sekondari school.
Ambapo ni umbali mkubwa sana kwa watoto wanaotoka kazole, cheta, magodani na kilongoni kwenda kupata elimu kwenye shule iyo, pia shule hii ya Honda secondary sio shule ya kijiji cha kazole pamoja na vitongoji vyake bali ni shule ya majirani zetu wa Vianzi.
Kwaiyo basi, kuna haja ya serikali ya kijiji kutenga rasmi maeneo yaliyotajwa pamoja na kuhakikisha yanatumika hipasavyo ili kuchochea ukuaji wa maendeleo ya kijiji.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment