Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KESI YA MAUAJI NCHINI KENYA KUSIKILIZWA TANZANIA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Kesi ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha inayowakabili raia wa Kenya waliotiwa mbaroni nchini Msumbiji na kuhamishiwa Tanzania miaka tisa iliyopita, itasikilizwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) Arusha Mei, 21, 2015.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mahakama hiyo mjini hapa jana, ilisema kesi hiyo ijulikanayo kama Onyango na wenzake tisa, wanadaiwa kutenda makosa hayo mjini Moshi na itasikilizwa kwa siku moja.

Wakenya hao wanadai katika maombi yao kwamba walikuwa nchini Msumbiji kwa ajili ya shughuli zao za kutafuta fursa za biashara, lakini walitekwa kinyume cha sheria na kuingizwa kwenye ndege ya kijeshi na kurejeshwa Tanzania, Januari 16, 2006 kisha kushtakiwa kwa mauaji na mashtaka mengine matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Pia mahakama hiyo itasikiliza maombi ya Mtanzania Mohamed Abubakari, anayepinga adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kutiwa hatiani kwa mashtaka mawili ya unyang’anyi wa kutumia silaha na Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Julai, 1998.

Maombi hayo yatasikilizwa Mei 22, 2015. Kesi hizo zitasikilizwa hadharani katika ukumbi wa Kibo, makao makuu ya AfHCPR yaliyopo kwenye jengo la ofisi za Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), eneo la Burka. Mahakama hiyo itafanya kikao chake cha 37 cha kawaida kuanzia leo hadi Juni 5, mwaka huu.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top