Leo katika kipindi cha Kero Yangu tuna angazia kwenye swala la wenye nyumba na wapangaji katika eneo la Mbagala Kipati mtaa wa Mangaya jiji la Dar es salaam.
Kiukweli kabisa wapangaji wamekuwa ni watu wenye kunyanyaswa sana na wamiriki wa nyumba, nyie wenye nyumba ebu kuweni na moyo wa uruma kwa wapangaji wenu jamani.
Maana vitendo mnavyo wafanyia wapangaji wa nyumba zenu havifai katika maisha ya leo, utakuta wapangaji mnachanga pesa ya kununua umeme kisha mkisha uweka umeme yatari mama/baba mwenye nyumba anatumia umeme huo kinyume na makubariano yenu.
Mfano wa matumizi ya umeme kinyume na makubariano ni kama kupasha maji moto au kupika chai kwa kutumia jiko la umeme, kuwasha fridge, kupiga pasi mda wote nk.
Mbali na hayo kuna baadhi ya wapangaji hushindwa kukaa kwenye baadhi ya nyumba kutokana na masharti ya nyumba hiyo kuwa magumu kupita maelezo, mfano wa masharti hayo yaweza kuwa ni kukatazwa kupika chakula kizuri kuliko mwenye nyumba, nk.
Ila ukiachilia matukio kama hayo, bado kuna tatizo la madarari kupandisha bei ya nyumba/vyumba ili waweze kupata malipo makubwa, bado tukumbuke ya kwamba mbali na wapangaji kutozwa kodi kubwa serikali hainufaiki na chochote kutoka kwa wapangaji mbali ya malipo ya ardhi kwa zile nyumba zilizo kwenye maeneo yaliyo pimwa.
Mkataba wa pango la nyumba ninayopanga unasema umeme ni Tsh 10,000 tu kwa mwezi, ila baada ya kuja mke wa mtoto wa mwenye nyumba matumizi yamekuwa makubwa kupita kiasi, pindi akisafiri waga umeme wa Tsh 10,000 unakaa zaidi ya siku 10, ila akirudi umeme wa pesa hiyoiyo 10,000 ni siku 4 tu.
Na hii ndio ilikuwa kero yangu, naitwa Zaituni Hally, kutoka Mbagala Kipati mtaa wa Mangaya. Wenye nyumba mbadilike maana sisi ndio tunao waweka mjini, mnatakiwa kutuheshimu na kusikiliza mawazo yetu maana hata sisi tuna aki ya kusikilizwa pia kama binadamu wengine.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment