Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga, amesema kuwa mfuko huo kutoa fedha kwa ajili ya kuziwezesha kaya masikini sio kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) bali ni mipango ya serikali kuleta unafuu wa kipato kwa wananchi wake.
Aliyasema hayo hivi karibuni katika kikao cha kazi kilichowashirikisha wadau wa mfuko huo kutoka Halmashauri za Mkoa wa Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Zanzibar wakiwemo waratibu wa TASAF wilaya na mkoa, waandishi, maofisa wafuatiliaji na wahasibu kwenye halmashauri.
Pia, Mwamanga alisema kuwa muungano waliouweka kati ya watumishi wa halmashauri na waandishi hao sio ‘ndoa ya mkeka’ bali ni endelevu lengo likiwa kuona wanashirikiana na kuufanya mfuko huo ulete tija kwa wananchi.
“Mpango huu unaofanywa na TASAF kugawa fedha kwa kaya masikini si wa CCM kama watu wanavyoghani, mpango huu ni wa serikali katika kuzikwamua kaya masikini kiuchumi na kuleta maisha bora kwa Watanzania wote,” alisema.
“Ili kuonyesha kinachofanywa ni kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, mpango huu umewashirikisha waandishi wa habari.
Muungano huu haujawahi kutokea, na waandishi msije mkadhani muungano huu kati yenu na sisi ni ndoa ya mkeka, bali ni jambo endelevu,” alisema Mwamanga.
Mwamanga alisema kwa kuwashirikisha waandishi kwa kina kwenye Mpango wa TASAF III ni kuwasaidia kuweza kuandika habari zilizo sahihi na wasikubali kupotoshwa na baadhi ya watu, ambao hawajui nia yao ni nini.
Alisema TASAF imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na ndiyo mradi mkubwa barani Afrika ambao umewezesha kuwafikia wananchi wengi, huku ukionekana jinsi unavyofanya kazi kuanzia matumizi ya fedha na uratibu wake, hivyo waandishi na wananchi ni vyema wauunge mkono.
Mratibu wa TASAF wilaya ya Lushoto, Beatrice Shemdoe, alisema kuwa wilaya yao imejipanga kunufaisha kaya za watu masikani 10,779 ikiwa ni kutoka katika vijiji 146 kwa kuziwezesha kupata uhakika wa chakula, gharama za matibabu na elimu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.
Share habari hii na wenzio wajue
Post a Comment