Wasanii wanaogombea ubunge mwaka huu wa 2015 nipamoja na:
1. Prof Jay- mikumi
2. Dude- tabora mjini
3. JB- kinondoni
4. Soggy doggy- segerea
5. Steve Nyerere - kinondoni
6. Afande Sele- morogoro mjini
7. Dokii- kilosa morogoro
8. King majuto- tanga mjini
9. Shilole- igunga
10. Kalapina- kinondoni
11. Mrisho Mpoto- ubungo
12. Juma chikoka-ilala
13. Kingwendu- hajaweka wazi jimbo
14. Wema sepetu- singida
Unaju mimi binafsi siamini kama wasanii ni watu serious katika utawala hakika, emagine msanii yeyote kati ya watajwa hapo juu anakua mbunge halafu anakuja kupata nafasi ya uwaziri kwa mfano kingwendu, wema, shirole na wengineo wote waliotangaza nia ya kugombea ubunge mnategemea nini??
Wataalamu mpo tu tena mmekaa kimya tuu kana kwamba hamuoni wala kusikia, ni vyema vigezo viwepo vya utawala kwa kweli bado akina Joti, mr.blue na wengineo woote wataingia bungeni kama wabunge au kwa nafasi zingine, ivi unadhani kati ya wote tajwa hapo juu wakiwekwa meza moja na mbatia wataelewana??
Tuwe wakweli jamani au wema awekwe na dk.slaa unategemea nini? au afande sele na tundu lissu wapi na wapi?? Lazima tuwe serious kiukweli bungeni sio kama kariakoo kusema kwamba kila mtu anafaa kuingia
Madhaifu ya katiba pendekezwa ya mh.sitta, kuwa mbunge ujue kusoma na kuandika tu. Ivi tujiulize siku wabunge wote au asilimia 98% wakiingia, hao wanaojua kusoma na kuandika obviously mawaziri pia tutakutana na hao hao watakao weka rehani rasilimali zetu na kutukejeli kwa lugha chafu kama mbuzi hula urefu wa kamba yake, ndege ya Rais itanunuliwa heri watu wale majani, fedha zetu za rada zitaitwa vijisenti na wanyama wetu watasafirishwa kwa ndege mpaka basi.
2 comments
ninaungana na mawazo yako ici lini tutajua maana ya uongozi?au mpaka wema awe wazir wa Elimu tuyaone madhara ndo tubadilike???Tanzania twafuatisha mitezamo ya nchi za mangaribi wakati hali zetu haziendani.TUBADILIKE WENYEDHAMANA.
ReplyHaa haaa
ReplyNa CCM wanaweza kuwapitisha tu maana na wao ni wasaniii
Post a Comment