Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

SOUTH AFRICA YAKANA KUMTOROSHA RAIS WA SUDANI

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.

Katika tukio hilo nusura rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.

Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe. Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.

Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
 
Kwa mujibu wa  gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka katiba.
 
Katika taarifa yake,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini humo.
 
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top