Benki Kuu imekanusha vikali kwamba sarafu ya shilingi 500 ina madini ndani yake hivyo ni mali inayoweza kutumika kutengenezea vito, kufuatia uvumi potovu ulioenea kila pembe ambao unawafanya wananchi wengine wanunue sarafu hiyo kwa bei mara tano hadi kumi y thamani yake.
Akiongea na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo, Meneja wa vituo vya Utunzaji wa Benki Kuu Bw. Abdul Dollah, amesema kwamba uvumi huo si kweli na kwamba katika sarafu ya shilingi 500 kuna madini machache mno ya nickel ambayo hayafai hata chembe kutengenezea vidani.
Amesema sio kweli kwamb sarafu za shilingi 500 hazipo katika mzunguko kutokana na kuhodhiwa na hao wenye kuvumisha na wanaotaka faida ya haraka haraka, na kwamba zinapatikana kwa wingi katika vituo vyake vyote.
Amesema huenda wananchi wanachanganya sarafu hiyo ya 500 na sarafu maalumu iliyotolewa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ambayo alikiri kwamba ina madini na thamani yake ni shilingi 50,000/-
Post a Comment