Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

UMRI MZURI WA KUZAA KWA WANAUME NA WANAWAKE NI KATI YA MIAKA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Mbegu za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa maswala ya uzazi nchini Uingereza, manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati huo na hivyo zinapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.

Daktari Kevin Smith, ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee Uingereza anasema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.

Dakta Kevin Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi. Daktari Kevin Smith ameorodhesha ugonjwa wa akili ''autism'', na ule wa kuchanganyikiwa ama ''schizophrenia'' miongoni mwa magonjwa mengine mengi.

Dakta Smith, anasema kuwa wizara ya afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ilikupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha. Maoni yake hata hivyo yanapingwa na muungano wa wauguzi wa uzazi ambao wanasema kuwa hilo halitakuwa suluhisho la kudumu.

Badala yake shirika hilo linaitaka serikali ya Uingereza iweke sera zitakazowasaidia waingereza waliofikia umri wa uzazi kupata ajira.

Manii yakivunwa mapema yatasaidia kuepuka maradhi mengi tu. Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini.

Akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The Journal of Medical Ethics, Dakta Smith nasema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo lakini kwa wale ambao wamegonga maiaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.

Profesa Adam Balen, wa shirika la British Fertility Society, ameonya kuwa mbegu ziliyohifadhiwa huwa hazina nguvu kama zile zinazotolewa moja kwa moja. Amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ilikuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.

''Kwa mtazamao hawa vijana wanahitaji ajira na wapenzi basi watapata watoto pasipo na matatizo yeyote.'' alisema Profesa Balen.

Wakati huo huo mwanasayansi mwenza Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao. ''ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30."
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top