Vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, wametakiwa kuimarisha miradi ya mfano inayokopesheka.
Rai hiyo ilitolewa na mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ester Riwa, katika semina ya ujasiriamali iliyofanyika katika Kata ya Monduli Juu.
Alisema Mfuko wa Maendeleo ya Vijana umekuwa ukiwawezesha vijana, hivyo wanatakiwa kubuni miradi ili waweze kukopesheka.
Ester aliwataka vijana kuwa na mwamko utakaowawezesha kujiletea maendeleo.Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Monduli, Rose Mhina, aliwataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kupata mikopo.
Alisema serikali inatoa mikopo kwa vijana yenye riba nafuu, hivyo wakati umefika kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo.
Hata hivyo, Ofisa Ushirika wa halmashauri hiyo, Ester Tarimo, aliwataka vijana kutumia fursa zilizopo katika kujiletea maendeleo.
Post a Comment