Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WAKULIMA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YAO

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Unapozungumzia tabaka la watu maskini hapa Tanzania, bila shaka utaanza kutaja wakulima. Wale wadogo wamekuwa wakiishi maisha duni licha ya kuwa na mashamba makubwa, hali nzuri ya hewa na nguvu kazi ya kutosha.

Mbali na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kama vile uhaba wa pembejeo za kilimo, wakulima wengine wanaishi kwa mazoea. Mfumo waliorithi kutoka kwa wazee wao ndiyo huohuo wanautumia mpaka sasa.

Uzoefu unaonyesha kuwa kama familia ilikuwa inazalisha magunia manane kwa mwaka, watoto nao watazalisha chini ya magunia 10. Kama familia ilikuwa inazalisha magunia 200, basi hata watoto wa familia hiyo watakuwa katika mkondo huo.
Maswali muhimu ambayo mkulima unapaswa kujiuliza kabla msimu haujafika ni kwamba unataka kulima zao gani, kwa ajili gani, utauza wapi, katika hali gani na faida yake ni kiasi gani kwa msimu mzima?

Ni muhimu kujua unataka kulima zao fulani kwa ajili ya chakula au biashara. Pia, mkulima unatakiwa kujua utauza wapi mazao yako. Jambo la muhimu zaidi ni kwamba utauza mazao hayo katika hali gani, yaliyosindikwa au kama yalivyo.

Wajasiriamali walio na ubunifu wamekuwa wakitengeneza fedha nyingi kupitia mazao yanayozalishwa na wakulima. Kwa mfano, mtu anakwenda kijijini kununua karanga kwa wingi. Yeye anazisaga na kuweka kwenye pakiti kisha kuziuza kwenye Supermarket.

Nakuhakikishia kuwa thamani ya karanga iliyotwangwa na kufungwa vizuri ni tofauti na ile iliyotoka shambani moja kwa moja. Kwa nini mkulima mwenyewe asifanye hivi kwa mazao aliyozalisha mwenyewe?

Kwa mfano, kama gunia moja la alizeti anauza kwa Sh50,000, kwa nini asikamue mafuta akapata lita 20, akauza na kupata Sh80,000 mpaka Sh100,000? Hii ndiyo njia pekee ya kuongeza thamani ya mazao.

Mkulima anayetaka kuinua kipato chake lazima atageukia njia hii na kuachana na kilimo cha mazoea ambacho kinamfanya ashindwe kumudu gharama za maisha. Mjasiriamali wa kwanza anatakiwa kuwa mkulima mwenyewe.

Ipo mifano ya wajasiriamali wengi ambao walikuja kuwa mabilionea wakubwa. Hapa Tanzania tunamfahamu Said Salim Bakhresa. Yeye anazalisha bidhaa nyingi za vyakula na matunda.
Ukiuliza historia yake utaambiwa alianza kidogokidogo mpaka kupata mtaji wa kuanzisha viwanda vya kutengeneza vyakula na vinywaji mbalimbali. Leo bilionea huyu anatambulika katika orodha ya mabilionea wakubwa barani Afrika.

Bilionea wa Mexico, Carlos Slim aliwahi kusema; vitu unavyovipenda vifanye viburudisho vyako, vitu wanavyovipenda wengine, vifanye biashara yako. Hapa alikuwa anamaanisha kuwa vitu wanavyovipenda wengine ni fursa kwako, ndiyo soko lako mkulima.

Mwanzo ndiyo changamoto kwa wengi wetu, lakini uthubutu ni jambo la msingi. Pia, tujifunze kwa wengine waliothubutu wakaweza. Sharti la kwanza la uthubutu ni kuwa na dhamira ya kufanya jambo na pili ni kuchukua hatua.

Siyo kila kitu utajifunza kutoka kwa mtu, mengine mazingira yanakutaka kufanya jambo fulani kulingana na utashi ulia nao. Mkulima mzuri lazima awe mtu wa kusoma na kujifunza kwa wengine waliofanikiwa kwenye kilimo cha kibiashara.

Ukifuatilia maendeleo ya viwanda huko Ulaya kuanzia karne ya 15 na 16, mapinduzi ya kilimo yalikuwa na nafasi kubwa kuchochea uvumbuzi na ugunduzi. Kabla ya mapinduzi ya kilimo, wakulima walizalisha kidogokidogo, baadaye wakaongeza mashamba ili kuzalisha kwa wingi.

Mazao yaliokuwa mengi, thamani yake ikapungua. Wakulima wakaanza kutafuta namna ya kutengeneza bidhaa za kuuza badala ya mazao yenyewe. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa kukua kwa viwanda Ulaya.

Ni muhimu leo wakulima wetu wakajifunza juu ya mapinduzi yaliyofanyika huko Ulaya Magharibi. Wakulima wenyewe walitumia fursa kuzalisha kadri ya mahitaji ya soko.

Pia, Serikali ina mchango mkubwa katika kusimamia maendeleo ya kilimo nchini kwa kutengeneza mazingira wezeshi. Takwimu zinaeleza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima lakini sekta hiyo inachangia kidogo kwenye Pato la Taifa.

Serikali ikiwawezesha wakulima ipasavyo, watakuwa na uwezo wa kuzalisha kwa wingi na kuongeza thamani ya mazao yao. Kwa hiyo, Serikali itaongeza mapato yake na wananchi wataweza kuuza nje bidhaa zao na kujipatia fedha za kigeni.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top