Habari zilizotufikia sasa hivi ni kuwa kuna mpango wa haraka unaandaliwa ili kutengua adhabu iliyotolewa kwa wabunge zaidi ya 35 kutohudhuria vikao vya Bunge.
Sababu hasa ni kuwa inavyoonyesha ni kuwa hata wale ambao hawana hiyo adhabu nao wameamua kususia ili kuwaunga mkono wenzao Katika kupinga kile kinachoitwa "Kuwakeketa wananchi kwa kutumia madaraka" na jambo hilo litakuwa la aibu sana kwa Bunge na Rais kuhutubia wabunge wa CCM Pekee ilihali nchi inajinadi katika jumuia ya kimataifa kama ya demokrasia ya vyama vingi.
Ikumbukwe pia hotuba ya kuvunja bunge kwa JK itakuwa kama ya kuhitimisha uongozi wake na mahusiano yake na mhimili huu Mkubwa(Bunge) unaowakilisha wananchi.
Kinachoogopwa ni picha gani itajengeka kwa mataifa pengine wahisani ukizingatia kutakuwa na mwaliko wa mabalozi na wawakilishi wa mashirika wahisani Ambayo yanatambua mchango wa vyama vya upinzani katika kutokomeza Ufisadi na uhujumu wa uchumi unaofanywa na viongozi wa nchi hii.
Kwa Sasa kete la October inaonekana kuwa zito kwa CCM, Nape alidai watatumia hata "Goli la mkono" Ila kwa mwamko mkubwa wa wananchi kwenye kujiandikisha "CCM inatoka SAA 12:00 Asubuhi." kuwatimua UKAWA bungeni, sasa October 2015, ni kuwatimua ccm Ikulu na majimboni.
Post a Comment