Baadhi ya wakazi wa Bunju wamevamia na kukichoma moto kituo cha polisi Bunju A baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto wakijaribu kuwatawanya wananchi hao waliokuwa wamefunga barabara baada ya mwanafunzi mmoja kugongwa na gari kisha kupoteza maisha yake pale pale.
Polisi walilazimika kukimbia na gari lao baada ya kuona wamezidiwa nguvu na wananchi, huku wakirushiwa mawe na kukiacha kituo bila ya ulinzi.
Kitendo cha polisi kukimbia kituoni hapo kilitoa mwanya kwa wananchi hao kuingia kituoni na kuwatoa wsarifu wote waliokuwa wameshikiliwa na polisi kisha wakakiwasha moto kituo hicho.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment