Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

HOFU YATANDA JUU YA KUHENGULIWA KWA JINA LA EDWARD LOWASSA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Taarifa za uhakika nilizopata toka kwa Team Lowasa ni kwamba wanajiandaa kukinukisha ndani ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM utakaofanyika Julai 10 Mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa mdau wangu ambaye yupo ndani ya Timu hiyo na ni miongoni mwa wanaoratibu mkakati huo, amesema kuwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ndiye atakayekuwa wa kwanza kuongea.

Kwamba, Nchimbi atahoji sababu za jina la Lowasa kukatwa katika hatua ya awali ili hali ana uzoefu wa kutosha kuliko wagombea wengine, anakifahamu zaidi chama, ana wafuasi wa kutosha ndani na nje ya chama na kubwa zaidi, amejizolea wadhamini wa kutosha katika mikoa 31 aliyotembelea.

Baada ya Nchimbi kumaliza kuongea, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa atasimama na kuunga mkono hoja hiyo. Slaa atasisitiza kuwa si busara Mkutano wa Halmashauri Kuu kuendelea huku kukiwa na sintofahamu ya sababu za mwanasiasa mkongwe, Edward Lowasa kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Sophia Simba naye atasimama na kuunga mkono hoja ya Nchimbi. Kwa mujibu wa mdau huyo, mjumbe mwingine atakayeongea na kuunga mkono hoja ya Nchimbi ni Sadifa Juma.

Baada ya wajumbe hao kuongea, wajumbe wengine ambao ni Team Lowasa watasimama huku wakishinikiza kutolewa maelezo yatakayowashawishi ya kuenguliwa Lowasa na kwamba endapo hawatapata maelezo yatakayowashawishi, watatoka nje ya kikao.


Nilipomuuliza endapo wajumbe hao watatoka nje ya kikao kinaweza kuendelea ama la, mdau huyo alisema kuwa mpaka sasa hawana hakika kama kuondoka kwao ndani ya kikao hicho kutazaa matunda.

Anasema kuwa awali Lowasa alikuwa na wafuasi wengi ndani ya NEC na MM ila kwa sasa wajumbe wengi wamedefect na huenda jitihada zao za kutoka hazitasaidia.

Ila amesema kuwa kabla ya kutoka, watahakikisha wanasoma mood ya kikao na ikiwa wataona kuwa wanaungwa mkono na wajumbe wengi ndipo watakapofanya maamuzi ya kutoka nje.

Nilipomuuliza sababu za Nchimbi kuteuliwa na Timu hiyo kuanzisha mjadala huo, mdau huyo kanidokeza kuwa Nchimbi ni mtu mkubwa ndani ya Timu yao.

Kwamba, kuna makubaliano baina ya mgombea wao wa Urais, Lowasa na Nchimbi. Kwamba, kwa mujibu wa makubaliano hayo, Endapo Lowasa atateuliwa kupeperusha Bendera ya chama na kushinda uchaguzi Mkuu ujao, atamteua Emmanuel Nchimbi kuwa Waziri Mkuu.

Aidha, mdau huyo kanidokeza kuwa Nchimbi ana hasira na Serikali hasa baada ya kuondolewa kwenye nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi kutokana na sakata la Operesheni Tokomeza.

Anasema kuwa Nchimbi aliamini kuwa baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo, angeteuliwa kushika wadhifa mwingine hali ambayo imekuwa kinyume chake. Hivyo Nchimbi anaamini kuwa ikiwa Lowasa atashinda, matarajio yake yatatimia.

Mdau huyo pia kanidokeza kuwa kwa mujibu wa katiba ya sasa, Waziri Mkuu lazima atokane miongoni mwa wabunge. Hivyo, kwa kuwa Nchimbi hana uhakika wa kushinda jimbo la Songea Mjini, Lowasa amemshauri kuwa akagombee jimbo la Nyasa ambako ana uhakika wa kushinda kwa asilimia kubwa.

Wadau, mkakati huu ni ishara kuwa Team Lowasa wapo maji shingo. Ni dhahiri kwamba mgombea wao amenusa kuwa anaweza kuenguliwa katika hatua za awali kutokana na kukosa sifa ila yeye anaandaa mazingira ili ionekane kuwa ameonewa.

Sasa tusubiri kuona maamuzi magumu yakichukuliwa na Lowasa baada ya kuondolewa kwenye mchujo wa awali.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top