Rais
wa Zimbabwe Robert Mugabe amekejeli uamuzi wa Amerika wa kuhalalisha
ndoa za jinsia moja katika majimbo yake yote 50 na kuapa kusafiri hadi
Ikulu ya White House kuomba Rais Barack Obama 'amuoe’.
Katika
mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini humo, Bw Mugabe alisema kwa
mzaha kuwa amepanga kuelekea Washington DC 'kupiga magoti mbele ya Obama
na amsihi akubali kuwa mke wake.’
Rais
Mugabe ambaye anafahamika kwa misimamo yake mikali dhidi ya ndoa za
jinsia moja, alikuwa anatoa maoni yake kuhusu uamuzi wa kihistoria wa
Mahakama ya Juu ya Amerika kuhalalisha ndoa za jinsia moja.
Akiongea
Jumamosi Rais Mugabe alisema, “nimeamua kwa sababu Rais Obama
ameidhinisha ndoa za jinsia moja na kupigia upatu ushoga, nitamtembelea
Washington, DC kumuomba awe mke wangu.”
Kwa ukali aliongeza, “Sielewi kwa nini hawa watu wanakiuka mafunzo ya Yesu ya kuonya binadamu dhidi ya kujihusisha na ushoga.”
Rais
Mugabe alishutumu serikali ya Amerika kwa kuongozwa na watu 'wanaoabudu
shetani’ na ambao ni aibu kwa taifa kubwa la Amerika.
Anaamini kwamba tabia za watu wa Luti zinazozungumzwa kwenye vitabu vya dini, zinafaa kukemewa kwa kinywa kipana.
Kulingana
na mtandao wa Naij.com, Rais Mugabe alisema japo Amerika imetawaliwa
kwa misingi ya Kikristo 'viongozi fidhuli wa kisiasa’ wanaongoza ili
kufurahisha nafsi zao.
Mugabe alitoa matamshi hayo tata saa chache baada ya maelfu ya wapenzi wa ndoa moja kufunga ndoa kufuatia uamuzi wa mahakama.
Mnamo Jumanne Mozambique, taifa jirani la Zimbabwe lilihalalalisha ushoga baada ya kubadilisha sheria za kikoloni.
Miezi mitatu jela
Uamuzi
huo wa Msumbiji ulitajwa kama ushindi mkubwa wa haki za mashoga ambao
waliondolewa kifungo cha miezi mitatu gerezani pamoja na kazi ngumu.
Sheria
za kikoloni zilizobuniwa mnamo 1886, zililenga mtu yeyote ambaye
'anajihusisha na tabia kinyume na maumbile’ lakini hakuna mtu
aliyewahishtakiwa tangu Msumbiji ijinyakulie uhuru 1975.
Mataifa
mengi ya Kiafrika yamepiga marufuku ushoga lakini Msumbiji imekuwa
'baridi’ kupinga haki za watu wanaotaka kuingia katika ndoa za jinsia
moja.
Kwingineko,
kinara mkuu wa chama cha upinzani cha Labour nchini Australia,
ameanzisha sheria inayokubalia ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, sheria
ambayo inapingwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi
huyo, Bill Shorten, amemtaka Bw Abbott kuwakubalia wanachama wa
serikali wawe na uhuru wa kupiga kura kuhusiana na swala hilo.
Abbot
ambaye ni mfuasi wa kanisa Katoliki alikataa kura ya uhuru wa ndoa za
jinsia moja na kusema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha uchumi na
usalama wa taifa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment