Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

KWANINI WEWE MWANAUME UNAKIMBIWA NA WANAWAKE? SOMA HAPA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Wewe mwanaume unayesoma hapa, jiulize; huwa unadumu na mwenzi wako? Unaachwa au kukimbiwa baada ya muda mfupi? Kama jibu ni ndiyo, hapa utapata tiba. Sikia nikuambie, wapo wengi ambao kila wakianzisha uhusiano, siku mbili tatu, mwanamke anamkimbia.

Anampenda sana, anamfanyia kila kitu ambacho yeye anaamini kinakidhi kwa mwanamke wake, lakini baada ya muda mfupi sana, anaachwa! Anabaki kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Rafiki yangu, lazima ujue kwamba pamoja na kuwa mapenzi hayana kanuni za moja kwa moja, zipo ndogo ndogo ambazo zikifuatwa, mateso kwako yatakuwa ni kitendawili.

Huwezi kukimbiwa na wanawake bila sababu za msingi, lazima kuna kitu kinachosababisha uachwe. Hapo sasa hakuna sababu moja, wewe ukiachwa kwa sababu hii, mwingine atakimbiwa kwa sababu ile. Katika darasa hili, ukijifunza kwa umakini utaweza kujua kasoro yako ilipokuwa na kufanya mabadiliko ili ‘usiachike’ tena!

Wanaume huwa wanawalaumu zaidi wanawake kutokana na sababu za hapa na pale zinazosababisha kuachana kwao. Lakini wengine hutoswa bila kuelezwa sababu za msingi.


Akibaki na maswali mengi lakini mwisho hupata msichana mwingine kabla ya kuachana naye tena bila kujua sababu halisi.Wakati mwingine sababu zenyewe huwa za maana lakini zingine mh!

Ni aibu kuzitaja hadharani. Hata hivyo, kuna wengine huamua kuachana na wapenzi wao kwa makosa ambayo wao hudhani ni makosa kumbe wao ndiyo wanaokosea! Hebu tuone…UKOJE?

Kama una tatizo la kuachana na wapenzi kila wakati, kipegele hiki kinakuhusu! Anza kuangalia tabia zako upya. Unaishije na mpenzi wako, jirani zako na watu wanaokuzunguka?

Unatumiaje ulimi wako? Wasichana wengi wanapenda wanaume wachangamfu na wacheshi wakiamini kwa namna moja ama nyingine, ni burudani kwao lakini huwa hawapendi kabisa uwachangamkie wengine kupita kiasi.

Wanaume wengi hupingana na hili lakini utafiti unaonyesha kwamba, asilimia 70 ya wanaume wanaowachangamkia sana wanawake, mwisho wake hufanya nao mapenzi kama siyo kuingia katika uhusiano moja kwa moja. 

Usibishe, tafiti uone!Kama una tabia hii, hata kama unaamini kwamba uchangamfu wako siyo wa nia mbaya kwa wanawake, achana nao maana unamkwaza mpenzi wako bila kujua. 

Wakati mwingine anaweza kuonyesha wivu lakini mwingine hawezi kusema, hivyo hubaki akiumia moyoni mwake lakini akichoka huamua kuachana na wewe hata kama anakupenda akihofia kuwa katika penzi la kuchangia. Angalia vizuri tabia zako katika kipengele hiki.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top