watu waliokisiwa kuwa majambazi wamekivamia kituo cha polisi stakishari ukonga. Kwa mujibu wa taarifa za awali watu hao wamevunja store ya silaha na kuchukua silaha zote aina ya SMG zilizopo kituoni hapo.
Hadi sasa polisi kadhaa inasemekana wameuwawa na jambazi mmoja aliyepigwa na risasi ya jambazi mwenzie. Jambazi aliyeuwawa inasemekana ni dereva wa bodaboda wa kituo cha njia panda aliyefahamika kwa jina la Madevu.
katika tukio hilo police 4 na raia 3 wamepoteza maisha.
Inasemakana majambazi hayo yametokomea na kuacha pikipiki 3, hali mida hii si shwari mitaa ya stakishari na maeneo ya karibu baada ya milio ya bunduki kutawala maeneo yote.
Walio wengi wamejifungia majumbani kwao na sasa hivi kelele za ving'ola vya magari ya polisi vinasikika stakishari yote. kwa habari zaidi tuendelee kusubiri hapo baadae.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment