Mawaziri wa fedha kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro wanakutana
kutathmini ombi la Ugiriki kupewa mkopo wa dharura baada ya mamlaka za
Athens kushindwa kulipa deni lake kwa Shirika la Fedha Duniani{IMF}.
Hapo Jumanne Mawaziri hao walikataa kutoa fedha za kuukwamua uchumi wa Ugiriki baada ya mazungumzo kuvunjika.
Ugiriki
imekuwa nchi ya kwanza katika Muungano wa Ulaya kushindwa kulipa deni
lake kwa IMF. Msukosuko wa sasa wa kifedha imezua hofu huenda Athens
ikalazimika kujiondoa kutoka kanda inayotumia sarafu ya Euro.
Mkutano wa Jumatano utaamua
ikiwa Ugiriki itapokea mkopo wa dharura. Aidha Ugiriki pia imeomba
kupewa fedha zaidi kuuchepua uchumi wake.
Katika kipindi cha miaka
miwili Ugiriki imepokea Euro bilioni 29.1. Mmoja wa washauri wakuu wa
serikali ya Ugiriki Elena Panaritis, ameambia BBC wanatarajia kupata
msaada wa fedha waliopendekeza kupewa
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment