Mwili wa marehemu ukiwa umepakiwa ndani ya gari ya polisi
Watu
wasiojulikana wamemuua mlinzi wa mahakama ya Kingulwira mjini Morogoro
kwa kumkata panga kichwani na kunyofoa baadhi ya viungo na kisha kutupa
mwili wake katika mashamba ya pangawe mjini Morogoro.
EATV
imefika katika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa umeharibika vibaya
huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa ambapo kwa mujibu wa
mashuhuda na ndugu wa marehemu wamesema mtu huyo alipotea nyumbani
takribani siku kumi na mbili zilizo pita hadi alipo okotwa na wachunga
ng`ombe akiwa ameuawa na mwili wake ukiwa umeharibika.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtaa wa tambuka reli Adamu Mwamganga amesema
amepata tarifa hizo kwa wachunga ng`ombe kisha kutoa tarifa jeshi la
polisi ambapo ameeleza marehemu alikuwa na ugomvi na ndugu zake kuhusu
mashamba huenda ndicho chanzo cha kifo chake .
Jeshi
la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuuchukua mwili wa
marehemu na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakati
uchunguzi bado unaendelea.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment