Hospitali ya wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga maarufu kama Jakaya Kikwete inakabiliwa na uhaba mkubwa wa wahudumu wa afya maji,dawa na vifaatiba hali inayohatarisha maisha ya wagonjwa wanaokuja kutibiwa katika hospitali hiyo.
Akitoa taarifa fupi mbele ya kamati ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii kaimu mganga mku wilaya ya Kishapu Dr.Peter Mwita amesema madaktari zaidi ya 12 wanahitajika katika hospitali hiyo lakini waliopo sasa ni 3 pekee huku akizitaja changamoto zingine ambao zinazorotesha utendaji wao wakazi.
Naye mkurugenzi mendaji wa tasisi ya Mkapa Foundation Dr.Elen Senkoro ameishauri Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kutumia mapato yake ya ndani na kuwashirikisha wadau wengine wa afya katika kuboesha huduma katika hospitli hiyo huku mganga mkuu wa koa wa shinyanga Dr.Ntuli Kapologwa akieleza mikakati iliyowekwa na uongozi wa mkoa kutatua changamoto zinazosababisha mdororo wa huduma za kiafya.
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hadima na maendeleo ya jamii Mh.Raphael Chegeni amesema wakati umefika kwa serikali kuhakikisha bajeti ya sekta ya afya inafanya kazi iliyokusudiwa ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na changamoto ambazo zinagharimu maisha ya watanzania.
Post a Comment