Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh.Charles Kitwanga amewataka wananchi visiwani Zanzbar kuondokana na hofu ya kuwepo askari wengi katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa marudio kwani wapo kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama wao.
Akizungumza na wananchi alipokuwa akitembelea katika maeneo mbali mbali ya kisiwani Pemba waziri huyo amesema amepata faraja ya kuwa wananchi wanaendelea na shughuli zao vizuri bila ya kubugudhiwa huku akikanusha taarifa za kuwepo kwa watu waliojificha katika misitu wakikimbia askari.
Mh.Kitwangwa aliwaagiza msafara umpeleke msitu mkuu wangezi ambapo aliambiwa kunawatu wamekimbilia huko na mara baada ya kufika alimtaka kamanda wa polisi mkoa Kaskazini na mkuu wakituo konde kuonyeshwa watu hao nakugundua kuwa hakuna ukweli juu ya uwepo wa watu hao na kuwataka watu kuacha kauli za kuwafanya watu waogope kuwa kunatatizo kumbe hakuna.
Baadae alitembelea kambi zilizofikia askari katika kambi ya FFU Mfikiwa mkoa kusini Pemba na FFU mkoa kaskazini Pemba ambapo mkuu wa mkoa kusini Pemba aliwataka askari waliopo kwenye makambi hayo kufanya kazi kwa uwadilifu ilikuhakikisha watu wanapiga kura pasi na kubughudhiwa.
Post a Comment