Wanawake wajawazito na wanaojifungua katika hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha wameitaka Halmashauri ya wilaya hiyo na serikali kutatua adha ya muda mrefu ya akinamama wanaojifungua kunyonyesha kwa zamu vitandani na kulazimika kusimama wima usiku mzima changamoto inayosababishwa na ufinyu wa majengo ya hospitali hiyo.
Wanawake hao walitoa kilio chao muda mfupi baada ya hospitali hiyo kupokea msaada wa vyandarua 446 vilivyotolewa kwa msaada wa wafanyakazi wa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii(NSSF) tawi la Arusha kama sehemu ya kupambana na ugonjwa hatari wa malaria kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo inayopokea wagonjwa takribani 10,000 kwa mwaka,huku wanawake hao baadhi yao wakionekana kusongamana vitandani na kudai kwamba licha ya kushukuru msaada wa vyandarua lakini changamoto hiyo pia inawaathiri kiafya.
Nae Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya hiyo Dk Ukio Kosirio akipokea msaada huo wa vyandarua amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kupunguza tatizo la malaria toka asilimia 30 hadi asilimia tano,lakini hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya damu na majengo ya wadi na sio vitanda ambayo ndicho chanzo cha msongamano wa kuwepo kwa malalamiko ya akinamama waliojifungua kulalamikia adha hiyo.
Post a Comment