Rais Kenyatta ametangaza kuwa Mirungi ni zao la kibiashara wakati alipokuwa akitia saini muswada unaotambua mirungi kuwa mmea wa kuzalishia taifa mapato kuwa sheria.
Rais Kenyatta pia ametangaza kwamba serikali yake itatenga dola za Kimarekani 10 milioni za kusaidia wakulima wa mirungi kwenye bajeti ya mwaka ujao wa kifedha.
Wakulima hao wameathirika sana kufuatia hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya kupiga marufuku uuzaji wa mirungi, maarufu pia kama miraa, katika mataifa hayo.
Hutumiwa sana na watu wa jamii ya Wasomali na hutegemewa sana na jamii zianzoishi katika maeneo ya mashariki ya Mlima Kenya, miongoni mwa watu wa jamii ya Wameru.
Pesa hizo zitatolewa kupitia Wizara ya Kilimo. Sheria hiyo itaifanya serikali kuweka mikakati ya kutangaza, kuzalisha na kusambaza na kuuza zao hilo.
Rais Kenyatta amesema kutaundwa pia jopo kazi la kuangazia changamoto zinazokabili sekta ya ukuzaji wa mirungi ambayo itatoa mapendekezo kwa serikali.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment