Jumla ya tani 78 za sukari ambazo zilisalimishwa na baadhi ya wafanya biashara wa kubwa wa sukari katika jiji la Arusha zimegaiwa kwa wananchi wa wilaya ya Arusha mjini ambao walikuwa wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa sukari .
Sukari hiyo ambayo ilisalimishwa na wafanyabiashara wakubwa ambao ni Neema Investment imegaiwa katika jumla ya kata 25 zilizopo katika wilaya ya Arusha mjini huku kila kata ikiwa inapatiwa mifuko 1000 kwa ajili ya wananchi wake .
Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Arusha ,Afisa tarafa wa kata ya Suye Felician Mtahengerwa alisema kuwa sukari sukari hiyo inayogaiwa kwa wananchi ni ile ambayo iliingizwa hapa mkoani na baadhi ya wafanya biashara wakubwa na kuisalimisha katika ofisi ya mkuuwa mkoa kama agizo lilivyotolewa .
Alisema kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha alisema kuwa mfanya biashara yeyote wa sukari ambaye anaingiza sukari mkoani hapa anapaswa kutoa taarifa katika ofisi yake kabla ya kufanya kitu chochote ikiwemo kabla ya kuuza sukari hiyo ivyo wafanyabishara hawa waliisalimisha sukari hiyo na ndio ambayo inagaiwa kwa kufuata utaratibu.
Alisema awali walishagawa sukari tani 45 na sasa ivi wanagawa tani zingine 33 ambazo zimetoka kwa mfanyabishara Neema intaprasesi ambayo yeye aliingiza sukari hii mara baada ya serekali kutoa agizo hivyo aliamua kuisalimisha kwa kutoa taarifa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na sasa ivi ndio wameigawa .
“kunautaratibu wa wafanyabishara wakubwa wanapoingiza sukar I tu hapa mkoani kutoa taarifa sehemu husika ili sukari ile iweze kugaiwa kwa kufuata utaratibu hivyo huyu alitoa taarifa na ndio maana tumekuja hapa kuungana nae kuakikisha kila kata inapata sukari mifuko 1000 ambayo itauzwa kwa bei halili ya serekali ambayo imeelekezwa”alisema Mtahengerwa.
Alisema kuwa utaratibu huu unaotumika wa kugawa sukari utaendelea hivi hivi na hata sukari ambayo imeagizwa na waziri mkuu iwapo itafika utaratibu huu huu ndio utatumika adi pale tatizo la sukari litakapo malizika kabisa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment