TFDA yaonya matumizi ya sukari ya kijiko kimoja
Wednesday, May 25, 2016
Mwanza. Wakati Serikali ikiendelea kukabiliana na changamoto ya uhaba wa sukari na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Ziwa, imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu matumizi ya sukari ya Kijiko Kimoja (KK).
TFDA walisema kutokana na kuongezwa ladha, sukari hiyo haifai kwa matumizi ya wagonjwa wa kisukari, wajawazito na watoto.
Hata hivyo, wafanyabiashara wamekuwa wakiondoa tangazo la tahadhari linalowekwa kwenye vifungashio na kuiuza sukari hiyo hasa wakati huu.
Akizungumza na wajasiriamali jijini Mwanza jana, Mkaguzi Mwandamizi wa TFDA Kanda ya Ziwa, Julius Panga alisema wafanyabiashara wanauza sukari hiyo kinyume na taratibu kwa kuondoa tangazo la tahadhari.
Panga alisema sukari ya KK ni tamu kuliko sukari nyingine. Mkazi wa Kirumba Mwanza, Maria Paskali alisema amelazimika kutumia sukari hiyo kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo uliopo.
“Nilimuagiza mtoto kwenda kununua sukari robo kilo dukani. Alileta sukari nyeupe ambayo ilikuwa ni tamu tofauti na ambayo nilikuwa nimeizoea,” alisema.
Maria alisema hakuwahi kusoma maelezo yaliyokuwa katika kifungashio.
Muuzaji wa duka lijulikanalo kama Mke Mwema lililopo Igombe Mwanza, Justin Ntahorija alisema hajawahi kuuza sukari hiyo lakini baadhi ya wateja wamekuwa wakiwatuma watoto na kuwapa maelekezo kuwa wasinunue sukari nyeupe.
“Juzi alikuja mtoto akitaka sukari lakini akanieleza kuwa, ameagizwa asinunue kama iliyokuwa kwenye kifungashio alichokuwa amekishika. Nilivyoangalia kifungashio nikakuta ni kile cha sukari ya Kijiko Kimoja,” alisema.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment