Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Kilimanjaro imekamata bidhaa kutoka nje za mamilioni ya fedha baada ya kuvushwa kwa njia ya magendo katika maeneo ya Kitobo, Kileo na Njiapanda zikisafirishwa kwa njia ya magari mawili na pikipiki tano.
Meneja wa TRA wa mkoa huo Bw. Abdul Mapembe ameiambia ITV kuwa, katika oparesheni hiyo ya kudumu wameyakamata magari mawili moja likiwa na usajili wa kenya likiwa na bidhaa hizo vikiwemo vifaa vya magari, televisheni. Pikipiki, simu za mkononi, nguo, mafuta ya taa, chumvi na sukari.
Bw.Mapembe amesema, wafanyabiashara wa bidhaa hizo baada ya kukamatwa walitakiwa wakalete vielelezo vya bidhaa zao kama wamezilipia ushuru mpakani kama walivyodai lakini hawajaonekana.
Kiongozi wa oparesheni hiyo Bw. Obednego Nicholaus amewaonya wenye magari na pikipiki hizo kuwa kama hawatajitokeza kulipia ushuru bidhaa zitataifishwa pamoja na magari hayo aina ya fuso na pikipiki.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment