Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza, imesimamisha huduma za usafiri wa vivuko vitatu vya kampuni ya Kamanga kuanzia leo hadi hapo wamiliki wake watakaporekebisha baadhi ya dosari zilizobainishwa na wakaguzi kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA).
Agizo hilo la kuitaka kampuni ya kamanga Ferry Ltd kusimamisha huduma za vivuko vyake kuanzia jumatano Mei 11 mwaka huu limetolewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella baada ya kutembelea katika kivuko cha Kamanga, akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.
Afisa mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Mwanza Kapteni Michael Rogers, Nusura naye atumbuliwe na mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza kwa uzembe wa kushindwa kusimamia maagizo yao, baada ya cheti cha meli ya MV. Orion kumalizika muda wake tangu Aprili 30 mwaka huu lakini kivuko hicho kimeendelea kutoa huduma kama kawaida.
Afisa masoko wa kampuni ya kamanga Sadi Abeid akaelekeza lawama kwa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA), huku katibu mtendaji wa chama cha kutetea abiria wanaotumia usafiri wa majini kanda ya ziwa Marcel Rugambwa akiunga mkono hatua ya serikali ya kuvifungia vivuko vya kampuni hiyo.
Mhasibu wa kampuni ya Kamanga Ambrose Kenzagi akajikuta mikononi mwa polisi kwa madai ya kukaidi agizo la SUMATRA, kufuatia wamiliki wa kampuni hiyo kuendelea kutoa huduma ya usafiri wa abiria kwa kutumia kivuko cha MV. Orion huku wakifahamu kuwa kina makosa 13 yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho.
Post a Comment