BREAKINGNEWS: Wabunge bila kujali itikadi zao za kivyama wametoka nje ya kikao cha Bunge baada ya Naibu Spika kukataa kauli ya serikali kuhusu wanafunzi wa Chuo cha Dodoma waliosimamishwa kujadiliwa. SAKATA LA UDOM LA LAZIMISHA BUNGE KUAHIRISHWA.
Kufuatua hoja iliyoletwa na Mbunge wa Kondoa na kuhitimishwa na Mwongozo aliouomba mh.Nasari juu ya bunge kujadiri suala la dhurula la wanafunzi wa UDOM kufukuzwa chuo,wakati serikali ndiyo iliyofanya makosa ya kutolipa mishahara ya walimu.
Wabunge walitaka suala ilo lijadiriwe bungeni pamoja na kusaidia wanafunzi kuwezeshwa kufika majumbani salama. Naibu spika kwa kutumia busara ya hovyo hakutaka suala ilo lijadiriwe.
Hali hiyo ilipelekea kuibuka kwa zomea zomea ya wabunge wa upinzani na kusimama kwenye viti vyao huku wakipaza sauti. Naibu spika akagiza wapinzani kutolewa kwa nguvu,kelele zilizidi hivyo yeye mwenyewe kuamua kuondoka ukumbini.
Bila kutamka kitu chochote huku akizongwa na wabunge walioonesha kutokubaliana namna anavyotumia vibaya busara ya kiti cha spika. Ulinzi mkali umeimalishwa viwanja vya bunge.
Source: Anatropia Theonest
Post a Comment