Ikiwa leo ni Juni 02, 2016. UONGOZI wa chuo kikuu cha Dar es salaam umetangaza kufuta ratiba zote za masomo chuoni hapo katika siku ya leo ambapo Rais Magufuli anatarajiwa kufika chuoni hapo kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maktaba ya kisasa.
Sambamba na hilo pia ratiba ya ziara hiyo ya rais Magufuli imebadilishwa sasa na baada ya kumaliza uwekaji wa jiwe la msingi katika maenwo ya Yombo ataelekea katika uwanja wa mpira wa Chuo hicho ili kuweza kuwahutubia wanafunzi hao na taifa kiujumla.
Taarifa za chinichini toka chuoni hapo zinasema kuwa huenda rais Magufuli akapokelewa na mabango yenye jumbe mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao huku suala la uhaba wa mabweni chuoni kufikia hata wanafunzi 10 kulala chumba kimoja kilichotengenezwa kwaajili ya wnafunzi wanne tu kulala.
Aidha, suala la kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wa UDOM, kusitishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge pamoja na kuchelewa kwa fedha za mikopo ya wanafunzi na kupelekea migomo yakitarajiwa kujitokeza katika mabango.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment