Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WATU 5 WAFARIKI NA 13 KUJERUHIWA MWANZA, CHANZO NI HIKI HAPA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Mnamo tarehe 28.06.2016 majira ya saa 7:00 usiku katika barabara ya Mwanza – Shinyanga eneo la Bushini kata ya Mabuki wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza, gari namba T.449 BCB aina ya Zhongtong mali ya kampuni ya Super Sami lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye William Elias Masa miaka [44] mkazi wa Mabibo Dar es salaam.

Basi hilo likitokea Dar es salaam kwenda Mwanza liligonga jiwe lililokuwa barabarani hali iliyopelekea dereva kushindwa kulimudu gari hilo na kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano [5] akiwepo Dereva wa gari hilo na msaidizi wake pamoja na majeruhi kumi na watatu [13].

Taarifa hiyo imewataja waliofariki kuwa ni dereva wa gari hilo aitwaye William Elias miaka [45] mkazi wa Dar es salaam, 2. Vaileth Odede miaka [21] mkazi wa mwanza, 3. Mwanamume mmoja na wanawake wawili wenye umri wa miaka 25-30 ambao majina yao bado hayajatambuliwa mpaka hivi sasa.

Majeruhi kumi na watatu [13] watano kati yao wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu na wengine nane wanaendelea na matibabu katika hospital ya wilaya ya Misungwi ambao ni 1. Sophia Miraji anayekadiriwa kuwa na miaka 20 hadi 25, 2. Kibilo Mwacha anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 hadi 40, 3. Boniphace Charles anayekadiriwa kuwa na miaka 38 hadi 40, 4. Frank Munyumi anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 hadi 30.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi.

Wengine ni 5. Stanley Zacharia anayekadiriwa kuwa na umri kati ya 25 hadi 30, 6. Sia Dauson miaka 28, 7. Hellen Leheke anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 35, 8. Michael Leonard miaka kati ya 30 hadi 35, 9. Kudra ibrahim mtoto wa miaka miwili na miezi sita, 10.

Zamda issa miaka 24, 11. Marietha Chrispher miaka 26, 12. Elizaberth Simon miaka 40 na 13. Dickson Msamba miaka 22. Majeruhi wote wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Inadaiwa kuwa dereva wa gari hilo alikuwa kwenye mwendo kasi, hali iliyopelekea kugonga jiwe lililokuwa barabarani na kusababisha dereva kushindwa kulimudu basi hilo na kupelekea kuserereka na kuanguka na kusababisha vifo na majeruhi. Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Misungwi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa watumiaji wa vyombo kuwa makini wakati wote pindi wanapokuwa barabarani, lakini pia kuacha kuendesha magari kwa mwendo kasi kwani kunapelekea ajali na vifo vinavyoweza kuepukika.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top