Kwanza kabisa mziki ulianzia kwa benk ya Crdb na wateja wake, watu walipata kuuliza maswali juu ya makato ya asilimia 18.
Majibu ya benki hii yalikuwa yanawachanganya wateja wake pamoja na umma kwa ujumla wake, maana ata kwenye tangazo waliokuwa wamelitoa mwanzo halikuwa na usahihi wowote juu ya kauri hii.
Hapo juu ni maelezo juu ya makato ya asilimia 18 ambayo yametolewa na The Citizen, ambayo yanaendana kabisa na maelezo ya Tanzania revenue authority (TRA) kama inavyo someka hapo chini.
Ukweli nikuwa kiasi cha tozo la ongezeko la thamani yaani VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya kiasi cha gharama za huduma iliyotolewa na benk au tasisi yeyote ya fedha.
Kwa mfano, Ada ya huduma ya benk ambayo ametozwa mteja ni Tsh 1,000/= kodi ya ongezeko la thamani itakayotozwa kwenye kiasi hiki ni Tsh 152.50 tu na benk husika itabaki na kiasi cha Tsh 847.50
Kiwango hiki cha shilingi 152.50 ndicho kitakachorejeshwa serikalini na benk au tasisi ya fedha baada ya kupunguza kodi ya ongezeko la thamani iliyolipwa kwenye manunuzi ambayo yamefanywa na benki au tasisi ya fedha husika.
Kwa mujibu wa sheria hii, kodi ya ongezeko la thamani VAT haitatozwa kwenye riba inayotozwa na benk kwenye mikopo.
Post a Comment