Zaidi ya wakazi 1100 waliokuwa wakiishi mtaa wa Maghorofa mengi manispaa ya Dodoma wameondolewa kwenye makazi yao kwa nguvu na mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA chini ya usimamizi wa jeshi la Polisi ambapo zoezi hilo limeacha simanzi na vilio kwa kaya 174.
Zoezi la kuwatoa wakazi hao kwenye nyumba hizo zilizoko kata ya Kikuyu Kusini lilianza mapema asubuhi likitekelezwa na kampuni ya udalali ya Mvina General Supply Limited kwa usimamizi wa Jeshi la Polisi.
Hata hivyo zoezi hilo almanusura liingie dosari baada ya baadhi ya vijana waliokuwa wakifanya vibarua kubainika kujihusisha na vitendo vya wizi lakini hata hivyo jeshi la Polisi lilikuwa macho na kufanikiwa kuzima majaribio yote ikiwemo la vijana wawili walioshirikiana kuiba fedha taslimu shilingi Milioni mbili na laki tisa ambao kamera ya ITV ilibahatika kuwanasa.
Zoezi hilo liliendelea ambapo wapo baadhi ya wapangaji waliondoa vitu vyao kwa hiyari huku wengine nguvu ikitumika ambapo kaimu katibu wa CDA Saidi Kamsumbile akisema limefuata taratibu za kisheria huku Mkurugenzi Mvina Ibrahim Kivike akidai awali kabla ya zoezi hilo walipewa notsi kuondoka ndani ya siku tisini na kisha kuwaongezea siku saba lakini hata hivyo walikaidi.
Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya wahanga wakiongozwa na Diwani wa eneo hilo wamelalamikia utaratibu uliotumika kwani umewasababishia hasara kubwa huku wakidai baadhi ya vitu vyao kupotea huku pia wakiua Mtaa ambao ulikuwa ukitambulika kisheria.
=============================
Ni tukio la aina yake, Wapangaji wa Nyumba za CDA maarufu kama "Maghorofani" wanatimuliwa muda huu, hii inatokana na lile Tangazo la hivi karibuni lililodai CDA wanataka kufanya ukarabati
Polisi wamejaa, ni taharuki tupu, hata kama mpangaji haupo wanavunja mlango vitu vinatolewa.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment