Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

WABUNGE MSIKUBALI KUUPITISHA MSWADA UNAOLENGA KUMZUIA MWANACHAMA KUTOCHUKUA MAFAO YAKE PALE ANAPO ACHA AU KUACHISHWA KAZI, YAFUATAYO NI MAONI YANGU.

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Jamani serikali isitake kututapeli sisi wafanyakazi, izi pesa tulizo zichangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni pesa zetu sisi wenyewe na ndio wenye kuzipangia matumizi.

Sioni sababu ya kuniwekea vikwazo kwa pesa ambayo nimeitolea jasho langu, na mkumbuke sisi watanzania tunalipwa mishahara midogo sana, watu makazini wanashinda njaa kila siku wanajibana ili kuona kama vimishahara vyao vinaweza kuwasogeza hatua moja mbele, hapo hapo kwenye ivyo vi mishahara vyetu vidogo tunalipa kodi pamoja na makato mengine

Leo hii mnataka kutuzuia kutochukua pesa zetu je mnamaanisha kitugani???

Je nani anajua siku ya ngu ya kufa?? jibu ni hakuna anayejua sasa kama hakuna anayejua inakuwaje haki yangu mnataka kuizurumu namna hii???

Macho yangu yote yapo kwenu wabunge nawaombeni sana msikubali kuupitisha mswada huu maana mkikubali mjue kabisa mnaenda kutengeneza Tanzania ya wezi na sio tena tanzania ya viwanda.

Upatikani wa kazi umekuwa mgumu sana, uwezi kupata kazi bila kuwa na mtu unayemjua ofisini hapo unapoomba kazi.

Je mtu akiacha au akiachishwa kazi leo alafu anakaa bila kazi wala pesa ya kuendeshea maisha yake mnategemea mtu huyu atafanya nini ili maisha yake yaendelee kama ilivyokuwa kipindi anafanya kazi????

Lengo la mifuko hii ya ifadhi ya jamii nikumsaidia mfanyakazi pindi anapo acha au kuachishwa kazi, sasa kama mnataka kubadiri maana hii mjiandae kwa kile kitakachotokea baada ya mswada huu kupitishwa na kuwa sheria.

Watu tunafanya kazi katika mazingira magumu sana alafu bado na vifuta machozi vyetu mnataka kuvichukua kisiasa jamani.

Hii sio haki kabisaaa maana hakuna mtu hata mmoja mwenye Garranty ya mimi kuwa nitafikisha miaka 60 na je kama nikifa kabla ya umri huo nani atachukua pesa yangu???  Hapa tusidanganyane kama mimi mlengwa nawekewa vikwazo juu ya haki yangu niliyo itafuta kwa jasho langu basi niwazi kwamba hakuna atakaye simama kudai haki yangu nikiwa niko kabrini.

TAMKO LA PAMOJA KATI YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII UNAOKWENDA KUZUIA FAO LA KUJITOA, [BOFYA HAPA TAFADHALI]

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top