Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii maalum iliyoandaliwa na timu ya habari ya (MTM). Leo tunataka kuwakumbusha wananchi wote kwamba ni wajibu wetu sote kujiongeza kwanza kimawazo na kifikra kisha ndipo tuje kuilaumu serikali yetu hii ya Tanzania.
Sisi wananchi tumekuwa tukifanya mambo mengi ambayo ni ya ajabu mno, na pindi tukimaliza kuyafanya mambo hayo tunakuwa wakwanza kuitupia rawama serikali.
Mfano wa mambo hayo nipamoja na Kuzaa watoto wengi bila mpangilio, kushindwa kuwapa haki zao hao watoto tunao wazaa, na moja ya haki hizo nipamoja na kuwapa miro ya vyakula bora, mavazi mazuri, elimu nzuri, huduma nzuri za matibabu, nk.
Tangu nazaliwa hadi kufikia umri wangu huu nilionao nimesikia maneno mengi sana na moja ya maneno hayo nipamoja na kuisifia nchi yetu ya Tanzania kuwa ni kubwa na ina mali na maeneo makubwa.
Sasa ebu tujiulize kati ya ukubwa wa nchi yetu hii, ni ukubwa gani umetengwa kwa ajili ya madini, wanyama pori (utalii), makazi ya watu, biashara, mito, maziwa, bahari, sehemu za maziko (makaburi) nk.
Mpaka sasa wanafunzi wanasomea chini ya miti ya miembe, huu sio mfano wa shule za vijijini bali ni mfano wa shule za mjini tena jiji la Dar es Salaam, nenda pale shule ya Mbagala kizuiani utajione mwenyewe ninacho kisema hapa. Je kama mjini hali iko hivi uko vijijini pakoje?
Na jambo hili si lakuilaumu serikali, bali nijambo la kuilaumu jamii nzima maana sisi wanachi tena wakipato cha chini ndio tunaochangia kwa asilimia kubwa maana tunazaa watoto wengi wakati hatuna uwezo wa kuwapa huduma zao stahiki.
Matokeo yake watoto wanakuwa wengi mitaani wakiwa hawajui kusoma wala kuandika, hawana kazi za kufanya, hawavai viatu wala kandambili, wanavaa nguo zimechanika, wanakuwa wezi, makahaba, nk. Chanzo cha haibu hii ni jamii na wala sio serikali kama wengi tunavyo paza sauti zetu tukilalamika.
Watanzania wengi vipato vyetu ni vidogo ukilinganisha na matumizi yetu, ukienda mahospitalini wazazi wanalalamika hawapati huduma nzuri, wengine wanatelekezwa wodini kisa hawajalipa madeni ya huduma mahospitalini humo hivyo hivyo hadi mashuleni wanafunzi wanalalamika juu ya madawati na mfumo mzima wa elimu kwa ujumla, alafu bado sisi wenyewe tunaolalamika ndio tunaendeleza ukubwa wa tatizo hili.
Lakini tukumbuke kitendo cha kutengeneza kizazi cha namna hii ni wazi kabisa na wao wanaendelea kuzalisha vizazi kama vyao na matokeo yake tunakuwa na taifa lenye watu wajinga na tegemezi. Je maendeleo yatapatikana kweli kama style tunayotumia ndio hii??
Pia kwa upande mwingine watoto hawa sio wakulaumiwa hata kidogo, bali anayestahili kulaumiwa tena kwa nguvu zote ni nyie wazazi mliokubaliana kuwazaa watoto hawa wakati mnajua fika hamna uwezo wa kuwahudumia ipasavyo.
Je hao watoto tunaoendelea kuwafyatua bila mpangilio watakuja kuishi wapi? Maana ukisema wataishi hapa nchini jua kabisa tunaenda kupunguza taratibu maeneo ya utarii, biashara, maziko, na kwingineko ili waweze kupata maeneo ya wao kuishi. Je kitendo cha kufanya hivyo kinakuwa na tija gani kwa maendeleo ya taifa???
Je serikali itaendelea kupanua maeneo ya wananchi wake kwa ajili ya makazi bila kuwa na maeneo mengi ya kuingiza mapato??? Yatupasa kufahamu ya kwamba hata ayo maeneo yatakayo punguzwa nayo yataisha tu kulingana na ukubwa wa watu jinsi wanavyo ongezeka, je yakiisha tutakuwa wageni wa nani??
Kuna aja ya serikali kuweka kikomo cha uzazi kwa watazania wote kama ni kuzaa mtoto mmoja au wawili, maana speed tuliyonayo sisi watanzania kwenye kuzaa ni kubwa mno kiasi kwamba inatishia amani na kuleta haibu kwa taifa, na tukiweza kuwa na kikomo cha uzazi basi maendeleo yatapatikana mara mbili na zaidi ukilinganisha na sasa.
Post a Comment