Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

AL SHAABAB WAVAMIA MSIKITI WA GARISSA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Viongozi Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuvamia msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa. Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni.

Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya. Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi.
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.

Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab.

Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom. Msikiti huo upo takriban kilomita 40km kutoka mji wa Garissa kulikotokea shambulizi la chuo kikuu mwezi uliopita.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walikuwa wameandamana na wapiganaji takriban 40 waliojihami tayari kwa vita. 

Mwandishi wa BBC Abdullahi Abdi aliyeko mjini Nairobi anasema kuwa serikali ya Kenya imeanza kujenga ua ilikuzuia mashambulizi kama hayo.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top