Ndugu mdau karibu sana kwenye ukurasa mpya kabisa unaoitwa Kero Yangu. Ukurasa huu utakuwa ukichapishwa kupitia Mutalemwa Blog live kutoka Dar pamoja na Tazama line.
Lengo la ukurasa huu nikutazama pale palipo sahaulika na kuwakumbusha wahusika ili wakapafanyie kazi. Pia ukurasa huu hauishii hapa Dar es salaam tu, bali mpaka mikoani.
kwaiyo kama kuna jambo ambalo halijawekwa sawa na wahusika iwe ni Serikali, watu binafsi au taasisi mbalimbali waweza kuwasilisha kero yako na sisi tutaichapisha mtandaoni ili iweze kupatiwa ufumbuzi wakudumu kutoka kwa mlengwa/walengwa/muhusika/wahusika.
Kwakuanza leo tuanzie kwenye barabara ya Kilwa (kilwa road), katika barabara hii kumekuwa na maoni tofauti juu ya watumiaji wakuu wa barabara hii ambao ni wakazi wa Temeke, Tandika, kwa Azizi Alli, Mtoni mtongani, Mission, Mbagala kuu, Mbagala rangi tatu, na maeneo mengine yaliyoko kwenye ukanda wa mwambao wa kusini.
Kuna kipande korofi sana ambacho kimeanzia eneo la sabasaba maonyesho mpaka Mtoni Mtogani. Kiukweli kipande hiki kina watesa sana watumiaji wa barabara hii, maana wanasema kwamba tangu kipande hicho kilipo kwanguliwa mwaka jana kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho mpaka sasa bado hakuna kilicho fanyika zaidi ya wakazi wa maeneo hayo kuoga vumbi wakati wa kiangazi huku magari yakiaribika nyakati za mvua kutokana na mashimo makubwa yaliyoko kwenye eneo hilo.
Kwaiyo jamani naomba kuungana na wananchi wote wanao tegemea barabara hii kama mkombozi wao tunaomba mamraka husika muweze kutatua kero hii kwa watumiaji wa barabara hii ya Kilwa maana ina wakwamisha katika mambo yao, mfano kuchelewa kazini nk.
Kwa maoni/ushauri au kero yako basi waweza kutuma ujumbe wako kwa sms au what's up kupitia 0659919292 kumbuka kutaja majina yako kamili na sehemu ulipo kisha ujumbe wako tutauchapisha na utawafikia wahusika.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment