Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

LIYOSEMA FILIPE NYUSSI RAISI WA MSUMBIJI

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Raisi wa Msumbiji, Filipe Nyussi ametaka uhusiano wa nchi yake na Tanzania ulenge pia katika sekta ya uchumi.

Nyusi alitoa kauli hiyo Dodoma jana wakati akihutubia Bunge ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza nchini tangu alipochaguliwa kuongoza Msumbiji. Uhusiano huu usiishie kwenye siasa, usaidie pia watu kusafiri ndani ya nchi hizi kwa urahisi sisi nchini kwetu tutaruhusu Watanzania waje kwa urahisi zaidi na wanapokuja wakae muda mrefu bila shida yoyote.
“Tungependa pia waje Msumbiji kufanya biashara wawasaidie pia watu wa nchini kwangu, kwa hiyo mbali na siasa tungepena kuekeleza uhusiano wetu katika sekta ya uchumi, utalii na elimu,” alisema. Alitaka raia wa nchi hizo mbili waishi kwa amani na kunufaika na uhusiano huo.

“Tulinde nchi zetu hizo mbili kwa kupigana vita dhidi ya ufisadi na ugaidi, vita ambayo dunia nzima inapigana nayo,” alisema Rais Nyussi. Alisema amefurahi kupata fursa ya kutembelea Tanzania na kulihutubia Bunge pamoja na kujifunza jinsi Bunge la Tanzania linavyofanya kazi ikiwamo jinsi ya kuendeleza demokrasia. 

“Bunge la Msumbiji linafanya kazi yake ikiwamo kutoa uamuzi mbalimbali wa Serikali, tunafanya kazi kwa pamoja ya kupiga vita ufisadi na sasa tuna kazi ya kuandaa bajeti,” alisema.

Alisema Msumbiji imekuwa na uhusiano mzuri tangu kabla ya Uhuru, uhusiano ulioasisiwa na Hayati Samora Machael na Mwalimu Nyerere. 

Alisema yuko Tanzania kuendeleza urafiki huo na kujifunza jinsi ya kuendeleza demokrasia. Akitoa salamu za shukrani, Spika wa Bunge, Anne Makinda mbali na kumpongeza Rais Nyussi kwa kuchaguliwa kuiongoza Msumbiji alisema Rais huyo ameweka historia kwa kuwa Raia wa kwanza wa Msumbiji kulihutubia Bunge la Tanzania.

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top