Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

ATIWAMBARONI KWA KUTAKA KUMLA URODA MTOTO WA DADA YAKE

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Jamaa mmoja, mkazi wa Gongo la Mboto-Mzambarauni jijini Dar ambaye jina lake halikufahamika amewekewa mtego wa nguvu kisha kunaswa akiwa katika harakati za kutaka kujivinjari na binti wa miaka 14, ambaye ni mtoto wa dada yake wa tumbo moja (jina linahifadhiwa).

Binti anayesadikiwa kurubuniwa na anko yake ambaye jina limehifadhiwa.

MCHAPO KAMILI
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo ‘anko’ huyo ambaye ni dereva wa magari ya benki maarufu jijini Dar, alidaiwa kumsumbua binti huyo wa sekondari kwa muda mrefu.

Ilisemekana kwamba, kwa mujibu wa binti huyo, anko wake alikuwa akimnunulia soda baridi na kumuahidi kuendelea kumfanyia hivyo endapo atakubali ombi lake.


Ilidaiwa kwamba, baada ya kuona usumbufu umezidi, binti huyo aliamua kukisanua kwa mzazi wake ndipo mtego bab’kubwa’ ukawekwa.

 MAKUTANO GESTI
Baada ya mzazi kumpa mbinu zote za kuhakikisha hajirahisishi kwa mjomba wake, alitakiwa kumseti ili aumbuke ndipo binti akakubaliana na mjomba huyo wakutane gesti (jina kapuni) iliyopo maeneo hayo ya Mzambarauni.


KIBANO
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, mjomba mtu akiwa anajiandaa ‘kumtoa kafara’ mtoto wa dada yake ndipo dada mtu na shemeji yake wakaibukia gesti chumba namba 02 na kuzua timbwili la kukata na mundu kwa kumtia mtuhumiwa mikononi kwa msaada wa polisi.
Baada ya kutiwa mikononi na baba wa mtoto wa kike, aliamua kumpeleka hadi kwa askari mmoja anayelinda benki na kumpaki gari kwa lengo la kumpeleka mtuhumiwa kwenye kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya Mzambarauni.

Hadi ‘shushushu’ wetu anaondoka kituoni hapo, jamaa huyo alikuwa akihojiwa huku akiomba suala hilo wakalimalize nyumbani.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top