YANGA iko katika hatua za mwishoni za usajili wa straika wa Zimbabwe, Donald Ngoma, lakini wakala na meneja wa zamani wa mchezaji huyo amewashauri wasijifikirie marambili.
Wakala huyo, Gibby Kalule, ambaye yuko nchini akisubiri kukamilisha usajili wa kiungo mpya wa Yanga raia wa Sierra Leone, Lansana Kamara alisema timu hiyo imekamilika kwa kuwa ina majembe kama Amissi Tambwe, Simon Msuva, Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Malimi Busungu lakini akitua Ngoma tu utasikia mayowe.
Giby alisema aliwahi kufanya kazi na Ngoma kwa kumpeleka Sweden kucheza soka, amesema Yanga ikijishauri itajikuta ikipishana na saini ya mchezaji huyo kwani ni mtu wa kazi ambaye yuko sokoni na kwa aina ya soka la Afrika anaweza kufanya kazi popote na akatisha.
Alisema Ngoma ni zaidi ya Didier Kavumbagu wa Azam anapokuwa kwenye boksi na ni mahiri kwenye kufunga kwa mashuti makali na hata vichwa.
“Sikuwa najua kwamba ni huyu Ngoma ninayemjua kuwa ndiyo Yanga wanataka kumsajili, wakifanikiwa kumpata watakuwa tishio sana kama atacheza sambamba na Msuva na Tambwe pale mbele yule kijana anajua kufunga,”alisema Gibby.
“Nilikuwa mshambuliaji wakati nacheza lakini nakwambia kwa jinsi ninavyomjua Ngoma hapa Tanzania akija nafikiri washambuliaji wa hapa watajifunza mengi kutoka kwake.
“Endapo Yanga watampata na kocha akafanikiwa kuwaunganisha pale mbele hilo litakuwa ni tatizo kwa timu pinzani, lakini pia Yanga wanatakiwa kuchangamka si rahisi kwa FC Platinum kumuachia kirahisi ni mchezaji bora pale, jamaa anajua sana, we utaona kama akija hapa.”
Enzi zake uwanjani, wakala huyo alikuwa mshambuliaji wa SC Villa na timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment