Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MAHUSIANO: MJALI MWENZI WAKO KULIKO CHOCHOTE NAYEYE ATAKUPENDA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Hiyo ni nidhamu kuu. Hapo unashauriwa kitaalamu kuwa mwenzi wako kama mtu ‘spesho’ zaidi wa maisha yako, unapaswa kwenda naye kwa maewaleno. Kusikilizana na kupeana muongozo wa kila siku katika maisha.

Fikiria kuwa una marafiki wengi, ndugu na jamaa mlioshibana lakini mwisho wa siku unapotaka kulala, hurejea nyumbani na kujifunika shuka moja na mwenzi wako. Bila shaka unaona ni kwa namna gani huyo anashikilia kipengele nyeti cha maisha yako.

Dunia katika pointi ya maradhi, hususan Ukimwi na magonjwa mengine ya ngono, ni yeye ndiye anayeweza kukuweka huru. Damu yako ikawa salama, kwani kinyume chake asipokuwa makini, anaweza kuchetuka, akachetukia maradhi, mwisho wa siku akakuletea gonjwa uhangaike nalo.


Kwa maana hiyo ni mlinzi wa maisha yako. Unalala fofofo karibu yake na mpo wawili tu chumbani, ukiamka hujikuti na jeraha lolote. Usipomjali mtu wa namna hiyo unataka thamani yake ukampe nani?

Kuna kundi la watu huwatanguliza marafiki kuliko wenzi wao. Yaani katika pande mbili, mwenzi wako anasema hili, halafu wewe unasikiliza neno la rafiki kwanza. Hilo ni kosa kubwa ambalo ni rahisi kuyeshusha upendo.

Ni bora unapoona mwenzi wako anaongea kitu ambacho unaona hakifai, utumie muda wako kumuweka sawa na akuelewe. Usithubutu kufanya kinyume chake kama hakuelwe. Mwisho kabisa, ukiona mwenzo ana wasiwasi, jiepusha na hicho anachokihofia au mfanye aondoe mashaka.

Mwenzi wako anahisi kuna mtu unatoka naye kimapenzi. Fahamu kuwa hilo linamtesa moyoni, huwezi kujua kaambiwa na wangapi mpaka akaja kukuuliza. Zifanye fikra zake ziwe huru kwa kumuelewesha mpaka aelewe au jiepusha na huyo mtu.
Mwandishi
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top