Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MSICHANA FAHAMU MAMBO 5 YA KUEPUKA MARA TU UNAPOCHUMBIWA

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.
Kuna mambo kadhaa ambayo msichana anatakiwa kuwa makini nayo katika kuhakikisha uchumba wake unadumu na kufikia hatua ya kuolewa na kwenda kuanza maisha mapya.

Yapo mengi lakini nitagusia matano ambayo kwa utafiti wangu ndiyo
yamekuwa yakiwafanya wengi wakimbiwe na wachumba wao na kuachwa wakilia.

1. Mazoea na wanaume
Wapo ambao wamejikuta wakiachwa solemba kufuatia tabia zao za kuwa na mazoea ya kijinga na wanaume.Yawezekana kabla ya kuchumbiwa marafiki zako wakubwa walikuwa wanaume (Wapo wanawake wa aina hiyo).

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba hakuna mwanaume anayefurahia ukaribu wa mchumba wake kwa wanaume wengine. Hata kama hakuna uhusiano wa kimapenzi lakini epuka sana kujichekelesha kwao, kuongozana nao, kukaa nao au hata kuwasiliana nao.Ukifanya hivyo utakuwa unamkwaza mchumba wako na inaweza kuwa moja ya sababu za kukuchenga.

2. Marafiki micharuko(Mapepe)
Ukishachumbiwa, kuna marafiki zako ambao ‘automatikale’ unatakiwa kuachana nao. Nazungumzia wale micharuko ambao hawawezi kukushauri vizuri juu ya maisha yako.


Hata wale ambao wamekuwa wakikushawishi kila wikiendi muende mkajirushe, baada ya kuchumbiwa unatakiwa kujiweka mbali nao ili kumpa amani mchumba wako.

3. Tabia za kisichana
Ukishachumbiwa wewe si msichana tena, utakuwa ni mama mtarajiwa wa familia yako. Tabia za kisichana kama vile kuvaa mavazi yasiyo ya heshima, kukaa vijiweni kuongea mambo ya umbeya na nyinginezo kama hizo hutakiwi kuendelea kuwa nazo.

4. Kujifanyisha
Alichokupendea huyo mchumba wako anakijua mwenyewe, kwa maana hiyo unatakiwa kuendelea kubaki wewe kama wewe. Usijifanyishe kwa namna yoyote kama ambavyo baadhi ya wasichana wamekuwa wakifanya.

5. Eti umeshaolewa
Kuolewa ni mpaka pale mtakapoingia kanisani, msikitini nk na kufungishwa ndoa. Kama bado hamjafika huko, wewe bado ni mchumba tu na hata kwenye ndoa unaweza usifike.

Kwa maana hiyo hutakiwi kuhamia kwa mwanaume kama ambavyo baadhi wamekuwa wakifanya. Unachotakiwa kufahamu ni kwamba kitendo cha wewe kuchumbiwa kisha kuamua kubeba virago vyako na kwenda kuishi na mwanaume ni kuwakosea wazazi.

Msomaji wangu, yapo mengi ya kuepuka mara tu unapochumbiwa lakini haya machache yanatosha kwa leo. Jiangalie tabia zako, zile ambazo unajua wanaume wengi haziwafurahishi, jiepushe nazo ili kumjengea mchumba wako mazingira ya kukamilisha taratibu za ndoa yenu.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top