Baada kimya cha muda mrefu hatimaye Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilibrod Slaa, anatarajiwa kufungua pazia la kampeni za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Dk. Slaa ambaye kwa sasa amepewa likizo na chama chake baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kujiunga na chama hicho, atafungua kampeni za Ukawa mkoani Dar es Salaam mwezi huu.
Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu zitaanza rasmi Agosti 22, mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chadema, John Mnyika, alidokeza kwamba Dk. Slaa atazindua kampeni za Ukawa katika Jimbo la Kibamba, ambalo yeye (Mnyika) anagombea ubunge kwa tiketi ya umoja huo.
Mnyika alidokeza hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na viongozi wa matawi na kata ya Goba, muda mfupi kabla ya kufanyika uchaguzi wa kura za maoni kumchagua mgombea udiwani katika eneo hilo.
“Dk. Slaa yupo mapumzikoni na jana nilizungumza naye kwa kirefu na aliniambia bado anapumzika, lakini atakuja kushiriki kampeni Jimbo la Kibamba ambalo mimi nagombea ubunge,” alisema Mnyika.
Hata hivyo, Mnyika alipoulizwa kama Dk. Slaa atashiriki kampeni za nchi nzima ama ataishia Jimbo la Kibamba pekee kama alivyozungumza naye, Mnyika hakutaka kufafanua zaidi.
Katibu huyo wa Chadema hajashiriki katika shughuli mbalimbali za Ukawa ikiwamo kikao cha Ukawa cha kumkaribisha Lowassa kwenye makao makuu ya Chama cha Wananchi (Cuf), mapokezi ya mwanasiasa huyo na mkutano mkuu wa Chadema uliompitisha kugombea urais kupitia Ukawa.
Hata jana Dk. Slaa hakuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la Cuf ambao ulihudhuriwa na viongozi wote wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa vya Chadema, Cuf, NCCR-Mageuzi na NLD.
Waliohudhuria jana ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Dk. Emmanuel Makaidi.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.

1 comments:
Namsubiri jumbo LA kibamba home.
ReplyPost a Comment