Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

TAHADHARI KWA WOTE WENYE MAGARI DAR

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Kuna mzee mmoja wa makamo hivi, hupenda kuvaa kanzu, midomo yake imeungua kidogo. Mzee huyu ni Mwizi au Jambazi.

Jinsi anavyofanikisha uhalifu wake: Huwa anavizia waendesha magari (mara nyingi kinamama) hasa yanapokuwa kwenye mwendo mdogo.

Yeye hujibamiza upande wa kushoto na kisha hujidondosha chini kwa kisingizio kuwa amegongwa, kutokana na kitendo hicho kuwa cha  ghafla sana, wanaoshuhudia na mwenye gari pia huamini ni ajali ya kweli!

Anaponyanyuka hufunua kanzu yake na kuonesha mirija ya mpira na mfuko wa sandalusi aliyofungwa kama mgonjwa wa kibofu cha mkojo na kudai yeye ni mgonjwa na alikua akielekea hospitali na umemgonga.

Hukutajia hospitali iliyo karibu na mahali "ajali ilipotokea" na kuelekeza apelekwe huko, na akiingia kwenye gari huandamana na kijana ama hudai fedha akajitibu mwenyewe.

Pia wakati mwingine hutoa bastola na kuwapeleka madereva eneo la Wazo Machimboni nyuma ya kiwanda cha saruji Ununio, kulikokuwa machimbo ya mawe zamani ambako sasa hivi kumebaki mashimo

Au madreva wengine upelekwa eneo la Mla Mlaleni nyuma ya Kongowe, na kuwapora kila kitu, pamoja na kuchukua funguo za magari.

Maeneo ya mawindo ya mzee huyo nikama ifuatavyo, jirani na Central Polisi/Railway Station, Posta Mpya, Jangwani kutokea club ya Yanga kuelekea Kigogo Darajani, Hospitali za  Mwananyamala, Temeke, Mnazi Mmoja, Ubungo Stand na Gongo la Mboto.

Mara nyingine mzee huyo hupenda kukaa njia panda/kona ya Barabara ya Migombani na ile ya Mwai Kibaki (old Bagamoyo road - Zantel).

SAMBAZA TAARIFA HII KWA WATU WENGINE.
                                   ^^^^^^^^

Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top