Featured

    Featured Posts

    Social Icons


Loading...

MGOMBEA URAIS AMPA USHINDI LOWASSA, SOMA ZAIDI

Maendeleo ya kweli na yenye tija kwa wengi yanaanzia kwako wewe binafsi, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya picha hii.

Mgombea urais ampa ushindi Lowassa
Mgombea urais Chama cha Tanzania Labour (TLP), Macmillan Lyimo amepingana na matokeo ya tafiti za

Mgombea urais kupitia Chadema Edward Lowassa akiwasili katika uwanja uliotumika kufanyia moja ya mikutano yao ya kampeni.

Dar es Salaam. Mgombea urais Chama cha Tanzania Labour (TLP), Macmillan Lyimo amepingana na matokeo ya tafiti za kisiasa yaliyotongazwa hivi karibuni na taasisi mbili, akisema kama Uchaguzi Mkuu ungefanyika Septemba, mgombea urais wa Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ndiye angeshinda kwa kishindo.

Mgombea huyo pia amedai tafiti ambazo matokeo yake yamekuwa yakitangazwa kuanzia mapema wiki hii zimekuwa hazijumuishi wagombea wanaoonekana kuwa ni wadogo, lakini akasema yeye ndiye atakayeibuka mshindi Oktoba 25 baada ya Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kumaliza kazi ya kuibomoa CCM.

Lyimo, ambaye alizindua kampeni zake mara mbili- Kilimanjaro na Dar es Salaam, alisema hayo jana wakati alipofika ofisi za Mwananchi jana mchana kueleza malalamiko yake kwamba wagombea wanaoonekana wadogo hawapewi nafasi kwenye tafiti, vyombo vya habari na midahalo, akisema mgombea wa CCM, Dk John Magufuli na Lowassa ndiyo wanaopewa nafasi.

Utafiti wa taasisi ya Twaweza unaonyesha kuwa kama kura zingepigwa kati ya Agosti 19 na Septemba 7, Dk Magufuli angeshinda kwa asilimia 65, Lowassa angepata asilimia 25, wakati utafiti wa Ipsos unaonyesha kama kura zingepigwa kati ya Septemba 5 na 22, mgombea huyo wa CCM angepata asilimia 62 na wa Chadema asilimia 31.

Akijenga hoja yake kuhusu Lowassa, Lyimo alisema tangu Aprili amekuwa akizunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya shughuli zake na kupata nafasi ya kuongea na wananchi kuhusu mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu.

“Ni ndoto za mchana kwa Lowassa kupewa asilimia 25,” alisema Lyimo.

Lyimo, ambaye amebobea kwenye masomo ya biashara na ambaye anadai amefanya utafiti kuhusu madini nchini, alidai kuwa tafiti hizo kuhusu uchaguzi ni za “kisanii”, akidai kuwa zinajibu kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliyesema chama hicho lazima kishinde kwa kuwa kina maarifa mengi.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo Agosti 4 mwaka huu kwenye ofisi ndogo za CCM zilizoko Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam wakati akimpokea Dk Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu baada ya kuchukua fomu za urais.

“Ratiba ya mabadiliko huandaliwa na Mungu si mtu. Wanachokifanya Lowassa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye ambao wametokea CCM, ni kukibomoa chama hicho maana ni agizo kamili kwa mujibu wa ratiba ya kimungu ya majira na wakati. Waliojenga ndiyo wanaojua kubomoa,” alisema.

Alisema tafiti hizo, ambazo alidai zinatolewa ili kuwaaminisha Watanzania kuwa Lowassa atashindwa na hivyo wasije kushtuka, zinaweza kuipeleka nchi kubaya na ikitokea hivyo taasisi hizo zitawajibika.

Lakini, pamoja na kumpa ushindi Lowassa kama uchaguzi ungefanyika mwezi huu, Lyimo alisema ana uhakika wa kumpiku na kuibuka na ushindi Oktoba 25.

Alisema Lowassa na Sumaye wakishamaliza kazi ya kuibomoa CCM, yeye ndiye atakayepanda chati na kushinda Uchaguzi Mkuu kwa madai kuwa amezaliwa “wakati nchi ikiwa imeshapata uhuru”.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Never let a problem become an excuse. Put your Problem in Proper Perspective. What is the secret ingredient of tough people that enables them to succeed? Why do they survive the tough times when others are overcome by them? Why do they win when others lose? Why do they soar when others sink? The answer is very simple. It's all in how they perceive their problems.

Share habari hii na wenzio wajue

Post a Comment

CodeNirvana
Powered by Blogger.
© Copyright Tazama Line
Back To Top