Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka majimbo matatu ya Makunduchi
na Paje huko Zanzibar na Lulindi Mkoani Mtwara kwa Tanzania Bara.
Akitoa matokeo hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstahafu DAMIAN LUBUVA amesema katika majimbo hayo katika wagombea wanane mgombea wa Chama cha Mapinduzi DR. JOHN MAGUFULI alikuwa anaongoza akifuatiwa na Bwana EDWARD LOOWASA,mgombea wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia CHADEMA chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.
Kwa mujibu wa matokeo hayo katika Jimbo la Makunduchi DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 8,400 sawa na asilimia 81 na Bwana EDWARD LOWASA alipata zaidi ya kura 1,700 sawa na asilimia 17.
Katika jimbo la Paje DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 6,000 sawa na asilimia 75 ya kura halali na Bwana LOWASA alipata zaidi ya 1,800 sawa na asilimia 23.6 ya kura zote halali.
Kwa upande wa Jimbo la Lulindi Mkoani Mtwara DR. MAGUFULI alipata zaidi ya kura 31,000 sawa na asilimia 71.2 ya kura halali wakati Bwana LOWASA alipata zaidi ya kura 11,500 sawa na asilimia 26 ya kura.
Source ITV
Post a Comment