18.00pm:Shughuli ya upigaji kura imekamilika kufikia saa kumi katika
vituo vyote vya kupigia kura vilivyoanza shughuli hiyo mwendo wa saa
moja asubuhi.
Hii ni kulingana na sheria ya uchaguzi nchini humo
ambapo inaagiza kwamba shughuli zote za upigaji kura zisitishwe ifikiapo
saa kumi jioni.Kwa sasa baadhi ya maeneo hayo yameanza kuhesabu kura
hizo.
17.27pm:Mgombea wa urais katika chama cha CCM John Magufuli
ametaka kuwepo kwa utulivu na kuwataka raia wa Tanzania kujitokeza kwa
wingi ili kupiga kura.
16.55pm:Tume ya uchaguzi nchini Tanzania
kupitia mkurugenzi wake imesema kuwa inatarajia kwamba rais mtarajwa
atajulikana tarehe 29 huku mipango ya kumpatia cheti cha kuchaguliwa
ikifanyika tarehe 30.
16.50pm:Katika kituo cha kupigia kura mjini
Dar es Salaam,afisa mmoja wa uchaguzi alionekana akiwapatia raia
makaratasi ya kupigia kura ambayo tayari yalikuwa yamewekwa alama ya
upigaji kura. Kulingana na mkurugenzi wa tume ya uchaguzi Kailima Kombo
afisa huyo tayari amekamatwa.
Kailima amesema kuwa watakuwa
wakitoa matokeo ya uchaguzi huo kwa awamu kuanzia hapo kesho saa tatu
asubuhi katika jumba la mikutano la Julius Nyerere.
16.29pm:Huko
Rukwa , Magari yaliokuwa yakisafirisha makaratasi ya upigaji kura
yalivamiwa na kuchomwa lakini tume ya uchaguzi iliweza kutuma vifaa
zaidi asubuhi.
Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania
Kailima Kombo amesema kuwa katika maeneo yaliothirika, muda utaongezwa
iwapo bado wapiga kura watakuwa katika milolongo.
Amesema kuwa
usiku uliopita maafisa waliokuwa wakipewa vifaa vya kupigia kura
,walitaka kuongezwa fedha ikilinganishwa na makubaliano yao.
Hivyobasi walichoma na kuyakata makaratasi ya kupigia kura na kukiwacha
kituo hicho bila kitu.Pia walichoma sajili za kupigia kura
15.22pm:Wakaazi wa kituo cha Kimara wanangojea makaratasi ya kupigia
kura kuwasili .Wazee na wasiojiweza wamelazimika kungojea kwa zaidi ya
saa nane kufikia sasa.
Zanzibar wapiga kura bila tatizo
15.12PM:Visiwani Zanzibar upigaji kura unaendelea kama kawaida pasipokiwa na dalili zozote zile za uvunjifu wa amani
15.12PM:Visiwani Zanzibar upigaji kura unaendelea kama kawaida pasipokiwa na dalili zozote zile za uvunjifu wa amani
14.33pm:Tangu asubuhi, wapiga kura hawa wa Kimara jijini, Dar es Salaam hawajafanikiwa kupiga kura.
14.00pm:Huko Dodoma: Katika kituo cha Majengoweyo,watu wengi wamepiga
foleni huku usalama ukiimarishwa.Wapiga kura waliohojiwa wamesema
wamepiga kura bila tatizo.
12.30:Katika kituo cha Meko, nje
kidogo ya mji wa Mwanza, kumetokea sokomoko, baadhi ya wakazi
wanalalamika kwamba majina yao hayaonekani kwenye daftari la wapiga
kura.
11.30am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha upinzani CUF,
Seif Sharif Hamad amepiga kura katika kisiwa kilichopo kisiwani Unguja.
11.00am:Baadhi ya wapiga kura waliojisajili katika maeneo mengine ya
bara wamelazimika kusafiri hadi maeneo hayo ili kupiga kura. Madereva
ambao hawakupewa siku ya mapumziko hawafurahii kwamba wasingeweza
kushiriki katika shughuli hiyo.
10.37am:Mgombea wa Urais kupitia chama cha CCM John Pombe Magufuli amepiga kura katika mkoa wa Kagera huko Chato
Ametoa wito kwa raia wa Tanzania kujitokeza kwa wingi ili kuwachagua
viongozi wanaowahitaji.Aidha amewataka raia hao kumtanguliza mungu na
kuweka amani.
Anasema kuwa alipopiga kura mvua ilianza kunyesha akisema kuwa ni ishara ya baraka.
10.00am:Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema kupitia UKAWA Edward
Lowassa ameongozana na mkewe katika kituo cha Arusha na kupiga kura.
9.36am:Mgombea wa Rais wa CCM, Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein,
akiwa katika chumba cha kupiga kura, kusini Unguja.Shein amewataka raia
kujitokza kwa wingi ili kushiriki katika shughuli hiyo ya kihistoria.
8.36am:Takriban wapiga kura milioni 22,750,789 wanashiriki katika shughuli hii ya kupiga kura hapa nchini Tanzania.
7.50am:Huku shughuli ya upigaji kura ikiendelea maeneo mengi yamesalia
kuwa mahame zikiwemo barabara na maeneo mengi ya mji wa Dar es Salaam.
Hii ni kwa sababu raia wengi wanashiriki katika shughuli ya upigaji
kura.
7.14am:Katika kituo cha Dodoma foleni ndefu imeshuhudiwa
,ni kituo kilichopo katikati ya mji.Baadhi ya wapiga kura waliofika
kituoni humo na kupiga kura wanasema hakuna tatizo lolote walilopata.
7.13am:Katika kituo cha kinondondoni tayari watu wameanza kupiga kura
bila matatizo yoyote.Sheria ya mita 200 inaonekana kuanza kuheshimiwa
kwani watu wanapiga kura na kuondoka vituoni
7.05am:Mtafarufuku
umetokeo katika kituo cha masaki baada ya maafisa wa uchaguzi kutoka nje
ya vituo vya kupiga kura na kuwaelezea raia kupanga mistari mitatu
inayowapendelea wanawake,na wazee. Wengi wa wale waliofika mapema
wamepinga hatua hiyo wakidai kwamba ni haki yao kupiga kura wa kwanza.
7.00am:Ni saa moja kamili saa za Afrika mashariki na wakati muhimu kwa
taifa la Tanzania ambapo shughuli ya upigaji kura inaanza rasmi
6.30am:Waangalizi wa kimataifa tayari wamefika katika vituo vya kupigia
kura katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania ili kushuhudia matukio ya
uchaguzi huo.
6.30am: Ili kutaka kufahamu iwapo jina lako liko
katika sajili ya uchaguzi wengi wamekuwa wakipiga nambari hizi *152*00#
pia ata wewe unaweza kupiga na kuangalia kama umesajiliwa.
6.15am:Usalama umeimarishwa katika kila kituo kulingana na maripota wetu wanaofuatilia matukio mabli mbali ya uchaguzi huu.
6.10am:Maripota wetu wamesambazwa kila maeneo ya taifa hilo ili kuweza
kukupatia habari za moja kwa zinazojiri katika maeneo hayo.
6.0am:Wengi wa watu wamewasili katika vituo hivyo mwendo wa saa kumi na
moja asubuhi ili kupata fursa ya kupiga kura hiyo mapema na kuelekea
majumbani mwao ili kufuatilia uchaguzi huo katika vyombo vya habari.
Raia waonyeshwa madebe ya kupigia kura ili wajue kwamba uchaguzi huo unafanyika kwa njia ya uwazi.
6.03am:Tayari maelfu ya watu wamejitokeza katika vituo mbali mbali vya
kupigia kura nchini humo ili kushiriki katika zoezi hilo linalotarajiwa
kuanza saa moja asubuhi.
6.01am:Ni asubuhi njema na siku muhimu
kwa raia wa taifa la Tanzania ambapo raia wanapiga kura kumchagua
atakayemrithi rais wa taifa hili Jakaya Mrisho Kikwete
6.00am:Habari ya asubuhi, Tanzania kuamua nani awemrithi wa rais Kikwete.
19:18pm: Waangalizi wa uchaguzi kutoka eneo la Maziwa Makuu wamesema wamefurahishwa na maandalizi ya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania imesema kuwa maandalizi ya shughuli hiyo yamekamilika asilimia 100
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment