Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha
tofauti kubwa katika idadi ya wanawake wanaovuta sigara wakiwa na mimba
nchini Uingereza, maeneo maskini yakiwa na idadi ya juu.
Takwimu
hizo zinaonyesha 20.2% ya wajawazito eneo la Blackpool huvuta sigara
katika kipindi cha ujauzito wao ikilinganishwa na 2.1 eneo la matajiri
la Westminister.
Kila mwaka zaidi ya mimba 70,000 huathiriwa na uvutaji wa sigara.
Kwa
jumla kiwango cha kadiri cha uvutaji sigara kimepungua chini ya
asilimia 11 nchini Uingereza lakini ripoti ya shirika la Smoking in
Pregnancy Challenge inapendekeza viwango hizo chini ya asilimia sita
ifikapo 2020.
Profesa Russel Viner wa chuo cha udaktari cha watoto
kiitwacho Royal Colledge Child Health amesema viwango vya uvutaji
sigara miongoni mwa wanawake wachanga wenye mimba imo juu zaidi
"Wana uwezekano mara sita zaidi wa kuvuta sigara wakiwa waja wazito wakilinganishwa na wanawake waliopitisha umri wa miaka 35.”
"Pia
tunajua kuna tofauti kubwa ya kikanda na viwango vya juu zaidi vimo
katika jamii fukara. Tunafaa kuchukulia suala hili kwa uzito."
Daktari
wa uzazi wa chuo cha Royal College of Obstetricians David Richmond
amesema ni muhimu sana kwa wanawake wajawazito kuacha kuvuta sigara
wanaposhika mimba.
”Hili husaidia kuboresha afya ya mtoto, kukua
kwa mtoto huyo na pia kupunguza matatizo ya ujauzito yanayoweza
kuepukika," amesema.
Siku zote bahati yako iko mikononi mwako tu, ili kudhibitisha kuwa ni kweli bofya kwenye picha iliyopo hapa chini.
Post a Comment